Peter Madukwa
JF-Expert Member
- Sep 20, 2012
- 3,139
- 2,488
Nachingwea; Lindi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majalilwa Majaliwa katika mwendelezo wa Ziara yake Mkoa wa Lindi ameweka jiwe la Msingi katika shule maalum ya sekondari ya wavulana Nachingwea inayojengwa katika kijiji cha Chiumbati nje kidogo ya mji wa Nachingwea.
Shule hiyo ya Sekondari inajengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo yanakusanywa kupitia ushuru wa mazao katika mfuko maalum wa elimu.
Kukamilika kwa shule hiyo inatarajia kuchukua wanafunzi 1600 kidato cha 1 hadi 6 hasa katika masomo ya Sayansi.
Shule hiyo ya kisasa ya bweni mpaka sasa imegharimu zaidi ya milioni 500 ambapo katika awamu ya pili baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Nachingwea limeidhinisha sh 480,000,000 kuendeleza ujenzi wa shule hiyo inayotarajiwa kugharimu sh bilioni 4.5 mpaka kukamilika kwake.
Akiongea na wananchi wa kijiji cha Chiumbati Mh Waziri Mkuu amewapongeza wananchi kwa ujenzi wa mradi huo ambapo amesifu ubora wa majengo yaliyojengwa katika kiwango cha juu.
Aidha Mh Waziri Mkuu amewasifu wananchi wa kijiji cha Chiumbati kwa kutoa ardhi bure kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ambapo ardhi hiyo ina thamani zaidi ya sh milioni 100 na kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa katika maeneo mengi si rahisi wanakijiji kutoa eneo la mradi wa ujenzi wa shule ya wilaya bure.
Katika ziara hiyo pia Mh Waziri Mkuu ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Naipanga, mradi wa barabara ya lami Nachingwea-Masasi pamoja na Mradi wodi binafsi ya kisasa katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea ambao pia unajengwa kwa mapato ya ndani.
Shule maalum ya sekondari ya wavulana ya Nachingwea itakuwa ya bweni na inatarajiwa kuwa na madarasa 32, chumba cha maabara ya kompyuta, jengo la utawala, nyumba 20 za wafanyakazi, mabweni, mini supermarket, zahanati, maabara ya chemistry na biology, uwanja wa michezo na huduma zingine zote muhimu ambapo mpaka sasa madarasa yaliyokamilika ni takribani 17, maabara 2, vyoo vya wanafunzi, na jengo la utawala.
Shule hiyo inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha 1 ifikapo January 2022.
Akizungumza na wafanyakazi Mh Waziri Mkuu amesisitiza uadilifu katika utumishi wa umma na matumizi ya fedha za umma na kwamba serikali haitavumilia watumishi wabadhirifu wa fedha za umma.