Nachomokaje hapa wakuu?

Nachomokaje hapa wakuu?

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Salam kwenu nyote.

Wakuu kuna rafiki yangu yupo Nyanda za Juu Kusini huko anafanya biashara. Last week alinipigia simu na kunijulisha kwamba amefuatilia sana till ya MPESA iliyo katika jina lake kule aliko lakini hajakufanikiwa ikabidi afuatilie Dar kwa njia za mkato ndio till ipo tayar bado kuichukua tu.

Sasa jana katika maongezi nikamwambia anipe mawasiliano ya mhusika ili nikamchukulie hiyo till tuagize kwa jamaa tunaofahamiana nao wanaokuja kubeba mzigo Dar. Leo jamaa kanitumia hadi nauli maana mimi nipo Dar na pesa taslimu laki moja ya kumpa aliyeandaa till, nimeenda nimechukua till maeneo ya maeneo ya Mbezi Makonde lakini kwa bahati mbaya nilipokuwa narudi nikawa nawasiliana na mtu wa kumpa hiyo till kwamba tukutane Ubungo.

Nimefika Ubungo till mfukoni hamna. Jamaa ananilaani sana.

Naomba wenye ABC za namna gani nifanye kusolve hili suala anipe.
 
Rudi ulikochukulia hiyo TILL ukamweleze kilichokupata atakuandalia nyingine kwa kutumia nakala ya till iliopotea kutokana na kumbukumbu wanazobaki nazo.
 
nenda kwa wakala aliekupa till muelekeze..anaiblock ya kwanza..anatengeneza nyingine...ingekua umefanya kihalali..ungechukua lost report alafu ndo ungepewa nyingine..mbona easy sana hio
 
nenda kwa wakala aliekupa till muelekeze..anaiblock ya kwanza..anatengeneza nyingine...ingekua umefanya kihalali..ungechukua lost report alafu ndo ungepewa nyingine..mbona easy sana hio

Wakala anagoma anasema kwa kuwa ilikuwa haijaanza kutumika inabid kutengeneza nyingine tu upya.
 
Jmn naombeni msaada nikipost tangazo zangu badae nikataka kuziona hizo tangazo nafanyj mbn nahangaika msaada mimj sio mtalam wa jamii forum

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakala anagoma anasema kwa kuwa ilikuwa haijaanza kutumika inabid kutengeneza nyingine tu upya.
mpe hela 30000 atakubali..akibisha nenda mlimani city hapo kwa jamaa mrefu mweusi atakusaidia
 
Back
Top Bottom