Nachukia kabichi!

machiaveli

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
2,225
Reaction score
5,055
Wakuu!

Yaani tangu nikiwa mtoto nimekuwa nikichukia mboga kabichi au sijui tunda,mzizi anyway
Nyumbani walikua wakipika iyo mboga lazima waniandalie mboga mbadala labda maziwa mgando au parachichi nk..

Mpaka nimekua 30+ siwezi kula kabichi nikila nahisi Kama vile nimekuwa ng'ombe aliyekatiwa mgomba anavyotafuna vile

Kila nikijaribu kumeza nahisi Kama nimekuwa mfungwa aliyeshikiwa bunduki analazimishwa ale

Ni Hali ya kawaida kweli?
 
Mdogo wako atakula vitu vingi amazing,sio kabichi asee
Hapo pa kumlisha vitu vingi amazing nimewaza ujinga, maana nowadays watu wanakula hadi vitu siyo vyakula..! Enwei, I'm out..!! 😂
 
Kabichi sio mboga ni kachumbari

Sipendi, hata ikipikwaje
 
Hahahaa.
Nilikuwa siipendi cabbage mpaka nilipojua kuipika, upate ka ubwabwa kako na virage pembeni, uwiiiih' mniache tu hapo hapo.!
Yaani home ilikuwa wakipika hilo wanasema kabisa leo bwana mkubwa tafuta mboga yako jiko hilo. Dude hata halieleweki lina ladha gani. Mara sukari sukari.
Rangi si kijani, si nyeupe si njano.
 
Yan ulivyo itaja tuu, najihisi tumbo limejaaa,hakuna kitu sipend kama iyo kabich hata niwe na njaa ya kufa sikulii hakiiii,, alafu kuna izo za kuitwa kunde sasa na choroko uuuwi n kisanga kabisaa nikihis harufu tuu kichefuchefu tayar
 
Hahahaa.
Nilikuwa siipendi cabbage mpaka nilipojua kuipika, upate ka ubwabwa kako na virage pembeni, uwiiiih' mniache tu hapo hapo.!
Tukianza kukuchunguza tutagundua kitu ndan yake haya baki hapo hapo hahaha
 
Mimi siipendi ila wewe ni noma. Mimi naweza kula tu ila siifurahii. Ni sawa na bamia na mrenda ni vitu nisivyopenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…