Nachukia kabichi!

Nachukia kabichi!

Nimegundua watu wengi hawalipendi Kabichi, sijui kwanini!

Labda inategemea na Mapishi.

Mimi sina ubaguzi wa vyakula, Kabichi la Mapishi yoyote yale nakula, hata lichemshwe kidogo tu na lisiwekwe nyanya na kitunguu, mimi nakula bila wasi wowote.

Liungwe, lisiungwe, kwangu shaka hakuna
 
Yan ulivyo itaja tuu, najihisi tumbo limejaaa,hakuna kitu sipend kama iyo kabich hata niwe na njaa ya kufa sikulii hakiiii,, alafu kuna izo za kuitwa kunde sasa na choroko uuuwi n kisanga kabisaa nikihis harufu tuu kichefuchefu tayar
Kweli watu hatufanani.

Kunde, Choroko/Chooko ziungwe kwa nazi na Wali ni hatari.

Uzuri wa kunde hata zikipikwa za Sukari iwe mboga ya kulia Chapati, Maandazi ni mlo mmoja safi sana.

Choroko/Chooko zichanganywe na Wali kwa jina lingine MSETO, nao ni mlo mmoja safi pia.

Kiongozi umeshawahi kula MSETO?

Je vipi MBAAZI, NJUGU MAWE, haziliki?
 
Hakuna kitu sipendi kama kabichi na njugumawe. Siipendi ile harufu yake
 
Twende mbele turudi nyuma
Ugali kabichi ni kula tusikufe tuu
 
Back
Top Bottom