Nachukia kuwaona wanamuziki wengi wa bongo flava wanapo perform live

Nachukia kuwaona wanamuziki wengi wa bongo flava wanapo perform live

yaani mtu unalipa kiingilio,

ukifika unaanza kupewa adhabu ya kuinua mikono juu Na kidole cha mwisho.

badala ya wewe uimbiwe, mic inageuziwa kwako wewe ndo uimbe.

msanii anapayuka tuu haupati Ile vibe ya mziki,

hatulii stejini, anakimbiakimbia Tu huku Na kule bila kuwa Na pattern ya mziki

mwisho wa siku unaanza kuulizwa maswali like "niimbe au nisiimbe?"

Ni Mara Mia waimbe playback Ili ilete Ile rhythm.

very stupid, hawa waandaaji Na wasanij Wao wamesahau kuwa hizo nyimbo washabiki wanazijua vizuri and kwenda kuwaona huko Ni kwamba Kuna kitu extra wanakitaka, Wao wanakimbiakimbia Tu stejini, very boring

ukitaka kwenda nao sawa labda ulewe kwanza
Eti niimbe au nisiimbe haha
 
Mm naona kupwaya kwa shoo ya jana labda coz domo hakuwepo maana angekuwepo yale matimu timu yangeleta mwamko kidogo leo tungesikia mara huyu kaaltupiwa makopoa Mara huyu kapigiwa buuuu
 
Mm huwa naendaga Kwenye dance tuu kama nataka live,huko Kwenye bongo flava sithubutu,..utaambiwa uinue mkono na upige kelelee hadi ukome na huyo anaekwambia hivo kashika suruali yake sehem ya zipu..basi ilimradi shida tuu..naishia kutusi moyoni tuu
 
Mm naona kupwaya kwa shoo ya jana labda coz domo hakuwepo maana angekuwepo yale matimu timu yangeleta mwamko kidogo leo tungesikia mara huyu kaaltupiwa makopoa Mara huyu kapigiwa buuuu
Sasa mkuu wakishatupiana makopo ndio kiiu yako ya muziki mzuri unakuwa umeshaikata au?
 
Jux sauti ilikuwa haitoki vizuri kama pumzi zinakata au labda sijui ni mic alipokuwa anaimba wivu.
--mimi nahisi vyombo vinavyotumika jukwaani sio vya kisasa--
 
Na nilichogundua jana ni kuwa mashabiki "wa kiba" si lolote kwa "msanii wao" kama HAYUPO DIAMOND, YAANI IKO HIVI HAPAKUWA NA MIKELELE WALA SHANGWE ZA KIVILE KWA KIBA KWASABABU HAJAKUWEPO WA "KUMLINGISHIA" ANGEKUWEPO DIAMOND NDIO WANGEJIFANYA WAO NI MASHABIKI WA KUTUPWA KWA KIBA.
 
hili swala la live limekua kama fashion ya mwaka huu
wabongo wakionelea kitu..
tulishazoea playback tuendelee tu
maana mtu anaimba bongo fleva kama akudo impact...
mimi binafsi live show sizipendi
vyombo vinapigwa vibaya, mambo vululu vululu
tuimbieni tu na cd muwe mnaimna sehemu kadhaa tunawaelewa...

hii fashion ya live waachieni wa hiphop jamani....
 
Yaani hakuna jambo linanikera kama kulazimishwa kunyanyua mikono.Eti mikono juu,mikono juu.Mara piga kelele!
Inaboa sana...hawajui tu....imba vzr ...onyesha ubunifu ....watu watanyanyua hyo mikono bila hata kuwaambia wapige kelele..
 
Hata ka barnaba kanajitahidi tu ila hao wengineo ni aibu tupu!
Jana nilijitahidi kupiga kodo mubashara lakini nguvu zangu za kustahmili ziliishia kwa dogo janja nikaamua kumwaga usingizi sasa sijui waliohudhuria tena wamesimama kama wacheza kwata huku kila msanii aingiaye anakuwa kamanda wao akiwaamrisha hiki na kile walikuwa na hali gani?
Hata jana ni kinyesi kitupu. Kila aingiae ni oyyoo nyingi na mikono juu huku msani akizunguka stejini mwendo ambao ukiuunganisha unamfikisha kariakoo na kurudi, na haimbi muziki kaachia waimbe mashabiki, wengine wakageuza ukumbi wa kujitambulisha kuwa wao ni xxl, watu wamekuja ku enjoy nyie mnapoteza muda kuleta ubishoo!!!
Kwakweli sijui wabongo tutajifunza lini, show iko miaka mingi lakini hakuna improvement yoyotee,
 
Back
Top Bottom