Nachukia Nchi yangu - Serikali ijirekebishe

Nachukia Nchi yangu - Serikali ijirekebishe

uttoh2002

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
17,060
Reaction score
32,400
Kwa kweli nachukia mambo yanayoendelea kwenye nchi yangu na uonevu mkubwa wa mifumo yetu.

Niwape pole sana kwa report mbaya ya CAG, ila pia niseme kisa changu kinachoula moyo wangu.

Nilikuwa nina safari ya Mbeya ya kikazi na gari langu, kweli ni my dream car na nimelinunua kwa gharama na jitihada.

Toka Dar kwenda Mbeya mnajua ni safari ndefu, nimeenda salama, nimeanza kurudi, wakati nakaribia Dar nikapata ajali iliyosababishwa na trafic.

Nimepita vizuri bila speed na sina ticket yeyote ya speed safari nzima, akawa anakuja mtu nyuma speed, jamaa wa tochi wakamwona.

Ili kufanikisha azma yao ya kumshika, wakanisimamisha mimi ghafla ili jamaa wa nyuma asimame, nikasimama, na ndipo gari la nyuma likaja na kunigonga.

Niliumia hata kushuka ilikuwa ngumu sana sana, gari limabaribika mno nyuma na sijui hata, pole sijuia maneno mengi, hayawezi nirudisha nilipokua.

Hemu trafic wetu hata kama mna tamaa, wekeni jicho kidogo la usalama, imagine ndo nipo na watoto kwenye gari?

Pamoja na kutuibia kodi zetu, kutuzulumu, kutubambia kesi, na mambo mengi mabaya mnayofanya, hemu sasa muuangalie usalama wetu kwa haki.

I am having a worse week of my life ndugu zangu....
 
Chuki zako Kwa traffic na Serikali Haina uhusiano wa moja Kwa moja na nchi yako
 
Pole sana sana. Ndiyo maana huwa tunasema ni jukumu la kila mmoja wetu kupigania mfumo bora wa uongozi ili tuondokane na hili janga la CCM. Au kama tunaipenda sana basi tuibane ibadilike. Mtu akikaa nyumbani kwa kudhani harakati za mabadiliko hazimhusu, ni suala la muda tu, kuna siku mfumo wetu mbovu utamwathiri kwa namna moja.
 
Back
Top Bottom