Kwani wewe pesa ulipewa na nani? Angalia hili suala la mkopo ni la kisheria labda utaweza kuwakwepa kwepa kama huna mpango wa kuajiriwa nchini na au huna mpango wa kwenda kusoma nje ya nchi.
Nina jamaa yangu alipata nafasi ya kusoma Ufaransa, alipokwenda kutafuta visa ubalozi wa Ufaransa akaambiwa apeleke document inayoonesha kuwa hadaiwi na loan board. Kwa hiyo elewa kuwa kila baada ya muda wanaexpand means za kuwabana loan beneficialies, na hivi vitambulisho vya uraia nazani hiyo na yenyewe itatumika kama njia ya kupata defaulters.