Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 778
- 1,592
Wadau kwema,
Wiki hii kumeibuka video ya kijana mdogo maarufu kwa jina la Kunku (Mtu wa kazi), ambaye ametrend mitandaoni baada ya kukutwa akiiba mbao zilizokuwa zikitumika kutengenezea mabango ya moja ya wagombea urais kuelekea uchaguzi wa Oktoba 2025. Kijana huyu, akiwa na sura ya uchovu na kukata tamaa, hakusita kueleza hadharani kuwa hana kazi na hali ngumu ya maisha ndiyo imemlazimisha kujihusisha na wizi.
Katika mahojiano yake na Manyunyu Tv, Kunku alionekana wazi akikiri kuwa kwa sasa wizi ndiyo “kazi” yake, akidai kuwa ndiyo njia pekee inayompatia kipato. Alienda mbali zaidi na kusema kwamba yupo tayari kukamatwa, kupigwa, au hata kuuawa kwa sababu hana namna nyingine ya kuishi. Kwa maneno yake mwenyewe, aliweka wazi kwamba kuacha wizi kwake haiwezekani kwa sasa.
View: https://youtu.be/YmViIe-_tBg?si=sZG_N9CQQjj6ri1y
Maneno ya kijana huyu ni ya kutafakari kwa kina. Tunapomuona akieleza bila woga kuwa yupo tayari kwa lolote ilimradi apate kipato, tunapaswa kujiuliza: kesho na keshokutwa atapewa kazi ya hatari zaidi, kama kuua mtu kwa fedha, atakataa kweli? Hii ni ishara ya wazi kwamba tunatengeneza bomu la kijamii litakalolipuka baadaye kama tusipochukua hatua mapema.
Binafsi naamini Kunku anahitaji msaada wa haraka, iwe ni ushauri, ajira, au msaada wa kifedha wa kumtoa kwenye hali aliyo nayo. Kijana huyu bado mdogo, na badala ya kumwacha aendelee kupotea kwenye wizi na hatimaye kugeuka kuwa jambazi sugu, wadau tunaweza kushirikiana kumsaidia akubali njia nyingine halali za kujipatia kipato.
Naomba kuwasilisha mjadala huu kwa wanajamii, hasa wale wenye nafasi, taasisi, au hata mtu binafsi mwenye moyo wa kusaidia. Tukimsaidia Kunku leo, tunaweza kuokoa maisha yake na labda pia maisha ya wengine wengi kesho.