Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 778
- 1,592
Akifingwa atanyokaKajichokea masikini, anaona bora afungwe akale ugali wa bure🙆♂️
Nchi inahitaji watu wengi zaidi wenye kuangalia mambo kwa undani zaidi kama weweWadau kwema,
Wiki hii kumeibuka video ya kijana mdogo maarufu kwa jina la Kunku (Mtu wa kazi), ambaye ametrend mitandaoni baada ya kukutwa akiiba mbao zilizokuwa zikitumika kutengenezea mabango ya moja ya wagombea urais kuelekea uchaguzi wa Oktoba 2025. Kijana huyu, akiwa na sura ya uchovu na kukata tamaa, hakusita kueleza hadharani kuwa hana kazi na hali ngumu ya maisha ndiyo imemlazimisha kujihusisha na wizi.
Katika mahojiano yake na Manyunyu Tv, Kunku alionekana wazi akikiri kuwa kwa sasa wizi ndiyo “kazi” yake, akidai kuwa ndiyo njia pekee inayompatia kipato. Alienda mbali zaidi na kusema kwamba yupo tayari kukamatwa, kupigwa, au hata kuuawa kwa sababu hana namna nyingine ya kuishi. Kwa maneno yake mwenyewe, aliweka wazi kwamba kuacha wizi kwake haiwezekani kwa sasa.
View: https://youtu.be/YmViIe-_tBg?si=sZG_N9CQQjj6ri1y
Maneno ya kijana huyu ni ya kutafakari kwa kina. Tunapomuona akieleza bila woga kuwa yupo tayari kwa lolote ilimradi apate kipato, tunapaswa kujiuliza: kesho na keshokutwa atapewa kazi ya hatari zaidi, kama kuua mtu kwa fedha, atakataa kweli? Hii ni ishara ya wazi kwamba tunatengeneza bomu la kijamii litakalolipuka baadaye kama tusipochukua hatua mapema.
Binafsi naamini Kunku anahitaji msaada wa haraka, iwe ni ushauri, ajira, au msaada wa kifedha wa kumtoa kwenye hali aliyo nayo. Kijana huyu bado mdogo, na badala ya kumwacha aendelee kupotea kwenye wizi na hatimaye kugeuka kuwa jambazi sugu, wadau tunaweza kushirikiana kumsaidia akubali njia nyingine halali za kujipatia kipato.
Naomba kuwasilisha mjadala huu kwa wanajamii, hasa wale wenye nafasi, taasisi, au hata mtu binafsi mwenye moyo wa kusaidia. Tukimsaidia Kunku leo, tunaweza kuokoa maisha yake na labda pia maisha ya wengine wengi kesho.
View attachment 3466646
Huyo atapelekwa jera miezi 6 alime na viboko juu akitoka ataanza kuona kazi halali na fursa mtaani aache uharifu.
Huyo unamwona amelewa bangi.
Jera ndo sehemu sahihi zaidi, maana ametamka wazi hana option nyingine ya kuishi zaidi kufanya uharifu ( wizi)Hata kupelekwa jela ni moja ya njia ya kumsaidia, vinginevyo huyu atakuja kuuwawa kwa kupigwa na wananchi ama kama sivyo basi atakuja kuua mtu ilimradi pesa ipo
I agreeJera ndo sehemu sahihi zaidi, maana ametamka wazi hana option nyingine ya kuishi zaidi kufanya uharifu ( wizi)
Akiwa jera atakutana na wataalam wa saikolojia watamfunza nidhamu na stadium za maisha na kumwandaa kuwa tayari kuishi katika jamii bila kutegemea uhalifu(wiz)
Mkuu,kama kila muhalifu ataangaliwa kwa jicho la huruma kama mleta mada anavyosema,basi tegemea kua uhalifu kuongezeka zaidi,Nchi inahitaji watu wengi zaidi wenye kuangalia mambo kwa undani zaidi kama wewe
Jera ni nyumbani kwa watu...yani kuna watu...bila kwenda jera awasikii raha...!Huyo atapelekwa jera miezi 6 alime na viboko juu akitoka ataanza kuona kazi halali na fursa mtaani aache uharifu.
Huyo unamwona amelewa bangi.
Mkuu,kama kila muhalifu ataangaliwa kwa jicho la huruma kama mleta mada anavyosema,basi tegemea kua uhalifu kuongezeka zaidi,
Hakuna justification yeyote ile yakuhalalisha uhalifu,
Uhalifu ni uhalifu tu,uwe una kazi au huna kazi,uwe na hela au usiwe na hela,uwe na njaa au uwe umeshiba,uhalifu ni uhalifu tu.
Ndio maana na mimi nikasema,msaada ataupata huko huko Jela kama wanavyoupata wenzake,yeye sio special kuliko wengine.Mkuu, hakuna anayesema uhalifu uhalalishwe. Uhalifu ni kosa na haubadiliki kuwa jambo sahihi kwa kisingizio chochote. Lakini pia ni vizuri tukatofautisha kati ya kuhalalisha na kutafuta suluhu ya mzizi wa tatizo.
Kumwangalia huyu dogo kwa jicho la huruma haimaanishi kumpa ruhusa ya kuendelea kuiba. La hasha. Inamaanisha tunakiri kuwa kuna changamoto kubwa za kijamii na kiuchumi zinazochangia vijana kuingia kwenye njia hizi mbaya. Tukipuuza bila kushughulika na mazingira yanayowasukuma, basi tutakuwa tunatengeneza majambazi wengi zaidi kuliko kuzuia.
Hata kumpeleka jela kwa mujibu wa sheria ni aina ya msaada pia, kwa sababu ni hatua ya kumzuia kuendelea na uhalifu na kumpa nafasi ya kurekebisha maisha. Mfano mzuri ni wale walioathirika na madawa ya kulevya kuwapeleka sober house si kuhalalisha matumizi ya madawa, bali kama njia ya msaada ya kuwakwamua. Vivyo hivyo, kijana kama huyu akipewa adhabu stahiki lakini sambamba na msaada wa kisaikolojia na kijamii, tunaweza kumbadili. Ndiyo maana nilisema huyu dogo anahitaji msaada zaidi kuliko kubezwa, si kwamba asiadhibiwe, bali adhabu iende sambamba na msaada wa kijamii unaomtoa kwenye mzunguko wa uhalifu.