Kama angekuwa msikivu na anayelitakia mema Taifa letu, angelifanya jambo moja kubwa kuliko yote:
Angesimamia mchakato wa kupata Katiba mpya. Katiba mpya ina tija kwa kila mtanzania wa leo na kesho, wa kila chama na asiye na chama, wa kila dini na kila kabila, wa bara na visiwani. Lakini kwa bahati mbaya, yeye na Serikali yake na chama chake, ndio wamekuwa kikwazo kikubwa wa kupata katiba mpya. Kwa hilo pekee, hastahili kusifiwa kwa lolote. Ataingia kwenye historia ya viongozi maadui wa ustawi wa Taifa.
Kama angelisimamia mchakato wa kupatikana katiba nzuri mpya, hakika angekumbukwa vizazi na vizazi, na angekuwa ameacha alama kubwa kwa Taifa lake. Lakini anacholifanya sasa ni sawa na fundi wa gari lililoharibika, lisilo na uwezo wa kutembea, lakini fumdi amekazana na kulipaka rangi.
Sent using
Jamii Forums mobile app