britanicca
Platinum Member
- May 20, 2015
- 18,261
- 48,864
Nimekuwa nafuatilia sana mataifa mbali mbali ya afrika na dunia kwa ujumla, Kwanza naanza kwa ku declare interest kwamba mimi ni mwana CCM, ambaye nimeitumikia CCM katika nyadhifa mbali mbali,ndani na nje ya nchi,
Nimeitumikia Tanzania ndani kipindi kidogo, ila muda mwingi nimeitumikia Tanzania nje ya afrika,
Kuwa mwana CCM hakunifanyi kuziba masikio na macho ili nisisikie maovu na kuyaona mabaya ya CCM,
Kumekuwa na utitiri wa visheria vinavyoongezeka kila siku na dhumuni lake si kumlinda mwananchi ila ni kumtisha mwananchi,
1.Sheria ya mtandao, ambayo imetesa sana watu wengi wanaotoa maoni yao, hasa yanapokuwa kinyume na serikali, lazima mwananchi atishwe lazima mwananchi abughudhiwe,
2. Sheria ya kukuta gari la Mtu limebeba baadhi ya bidhaa na kulitaifisha, na kulipiga mnada, siyo kabisa, watozeni faini na muwarudishie magari yao,
3. Sheria ya mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya kumuweka Mtu yeyote ndani bila uchunguzi au kupitia kamati yeyote, huu ni uonevu wa hali ya juu sana, maana watu hasa viongozi so malaika wana matatizo n.a. wana maadui hivo wengi hutumia fursa hiyo kuwakomoa maadui,
4. Sheria ya kodi au ukokotoaji wa kodi, Tanzania ni nchi ambayo ina kiwango kikubwa cha kodi kwa afrika mashariki na ni ya pili kwa afrika nzima, utitiri wa kodi kwa kila hatua, wafanya biashara mnawakatisha tamaa sana, na pengine mnanadi bidhaa zao kwa kuwakomoa na kuwaonea,
5. Kumiliki blog au YouTube chanel eti mpaka ulipie kodi hiki ni kituko cha karne , yaan ni hatari, nchi zote watu wana YouTube channel na blogs hata website ,hawapelekeshwi kama huko Tanzania, nimeshangaa sana mpaka sasa kina Shaffy dauda wamewekwa ndani kisa kumiliki YouTube channel,
6. Tanzania inaprolong process za kuwapatia watanzania vibali vya kusafiria , na ni kama vile passport siyo haki ya mtanzania, wanauliza uLiza unaenda wapi, kwani ni mpaka nisafiri mda huo? Wenda naitafta mapema kujiandaa na safari za mbeleni
7. Kuna baadhi ya mazao Tanzania mkulima huna mamlaka ya kuuza mavuno yake mpaka uuzie ushirika, ukithibitika umeuza kahawa kwa rafiki yako unafungwa, huko ni kagera,
Yaan Tanzania tunawatesa wananchi
Britannica

Alafu na wewe hazikutoshi unasahau vipi ya KUPITA UWANJA WA NDEGE MPAKA UONESHE MKATABA WA UGHAIBUNI UNAPOFANYA KAZI
Umesahau sheria ya dereva kutembea na cheti cha masomo ya veta yaan ni upuuzi
Tena kumbukeni mnapaswa kumiliki laini moja ya simu
Umesahauuuu sana huruhusiwi kutoa takwimu hata ya umri wako kwenye mtandao, hata idadi ya wanafamilia sheria ya takwimu inakubana,
8. Sharia yakutopinga matokeo ya uchaguzi wa raisi
9. Sharia inayo kataza raisi kutoshitakiwa akimaliza uongozi wake.
10. Sharia inayo mpa mamlaka raisi kuteua wa kuu wa mikoa wilaya na ma DED bila kua veted na Bunge.
11. Sheria inayo mruhusu mwana jeshi kuchukua waadhifa wa kisiasa wakati haja staafu jeshi.
Kuna sheria inamtaka msanii akifanya show mwenye ukumbi analipa pesa BASATA kwa hiyo show.
Sheria zote hizo kandamizi zinapitishwa kwa kura ya "ndiyooooooo" inayopigwa na wabunge wa CCM.
Sasa wabunge wa CCM wanapitisha sheria ya walimu wote kusajiliwa,
Kuna sheria mahususi kuivuruga Tanganyika Law Society inapitishwa na wasomi kina Kabudi na wabunge wa CCM wakiwa wameshupaza shingo kama mbao.
Yaan Tanzania tunawatesa wananchi
Britannica