Katika nchi ambayo ina utamaduni wa hewala hewala, mtoto akikulia utamaduni huo, hata akija kuwa msomi anakuwa nsomi wa hewala hewala.
Na akishika nafasi ya juu kabisa anajiona mfalme. Kila mtu ampe hewala hewala.
Ndiyo maana watu wanalalamika lalamika wakuu wa mikoa na wilaya wanatumia sheria za kukamata watu vibaya.
Lakini hapo hapo ukisoma sheria unayompa mkuu wa wilaya au mkoa nguvu za kufunga watu, chini yake kunansheria inayosema mkuu wa wilaya au mkoa akitumia madaraka vibaya kifunga watu aadhibiwe vipi.
Nani kaanzisha kesi kumshtaki Mkuu wa Wilaya aliyetumia madaraka vibaya?
Jitu linasoma mpaka PhD, linakuwa libunge na liwaziri miaka kibao, linafika uongozi wa juu kabisa wa nchi, linashindwa hata kuongea kwa staha za uongozi wa juu kabisa wa nchi tu.
Na watu wanalishangilia, jembe.
Hapo tatizo si usomi tu.
Usomi wetu unaelea kwenye utamaduni wa ushamba na kuabudu wakubwa bila kujali wanayofanya.
Ndiyo maana watu wanaoweza kupinga mabaya ya wakubwa ni wachache sana.
Usomi ambao haujaweza kusaidia mtu kuwa na staha ndogo tu, ni magumashi.