Nadhani sheria hizi ziko Tanzania tu na zinamkandamiza mwananchi

Kuna sheria inamtaka msanii akifanya show mwenye ukumbi analipa pesa BASATA kwa hiyo show.

Sheria zote hizo kandamizi zinapitishwa kwa kura ya "ndiyooooooo" inayopigwa na wabunge wa CCM.

Sasa wabunge wa CCM wanapitisha sheria ya walimu wote kusajiliwa,

Kuna sheria mahususi kuivuruga Tanganyika Law Society inapitishwa na wasomi kina Kabudi na wabunge wa CCM wakiwa wameshupaza shingo kama mbao.
 
Mkuu hizi sheria ulizotaja wanaCCM wakisoma watasonya watataka tufunge huu mjadala.

Umezigusa sheria mbazo ndiyo uti wa mgongo wa CCM.
 

Umeongea maneno mazito
 
1. Si kila mtu kawachagua wawakilishi hao.

2. Mwananchi kulalamika ni sehemu ya demokrasia.

3. Hapa watu wanalalmika kama wananchi. JF motto we dare to talk openly. Wewe ni nani unahoji wanachi wanavyolalamika?
Kabisa na umesema la maana
 
Sheria tumetunga wenyewe kupitia wawakilishi tuliowachagua wenyewe (wabunge). Wewe unalalamika kama nani? Hazikuhusu. Nani kakwambia tunatakiwa kutunga sheria zinazofanana na nchi za wengine?
 
Yaan Tanzania tunawatesa wananchi
hakuna uhuru usiokua na mipaka
Hata huko US walifungia Al jazeera,UK wamekwaruzana sana na gazeti la Al Quds
Ukitaka kujua wanatesa wananchi angalia hali za weupe na weusi au ukitaka kujua kua US wanaminya haki ya kutoamaoni bas Mualike Louis Farkkan
 
Hivi ni sheria gani ile inayokataza kusema "rais kitu gani?" Ukisema tu, ndani miezi sita! Ukimsema naibu spika-----sijui naye itakuwa miezi sita ndani? Ukimsema Mbowe je? Au hii ni sheria maalum kwa watu maalum.

Ooh, Tanzania, Tanzania, Tanzania. Unavurugwa mama!

Britanicca wa CCM mwenye akili inayo-'charge'. Haya yote huwa unayatoa wapi? Bila shaka wewe ni masalia ya CCM ya Mwalimu!
 
Umesahauuuu sana huruhusiwi kutoa takwimu hata ya umri wako kwenye mtandao, hata idadi ya wanafamilia sheria ya takwimu inakubana,

Tutacheka, lakini ukweli ndio huo!
Ole wako uwe unatafutwa kubambikiziwa kesi, mashtaka hayo ni halali kabisa kukuweka ndani.
 
kweli kweli na hili swala litaendelea kama watu wasipo vungua macho nakuona nini kinachoendelea
 
mda mwingine kwenye kodi naona is such overated kiasi kwamba inakuwa dhulma ndio maana hatuendelei
 
Shida kubwa ni wasomi na wataalamu wa Kitanzania wapo static(mawazo mgando) ,wanapaswa kubwa dynamic (waendane na wakati na mahitaji).
Balaa kubwa tena siasa mawazo ya mtu mmoja mkuu anaeweza badili mifumo kwa kauli zake.
Duh,kweli aisee,sheria zimekuwa nyingi mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…