Nadhani Simba waache ujinga wa "sijui pira biriani"

Kwahiyo ninyi hamtaki kufungwa?

Yaani mkifungwa tu nongwa acha utoto basi.
Yaan hizi timu zetu za simba na yanga ni shida. Zikifungwa tu ai kutoa sare wanaanza kutafuta mchawi.

Hivi mbona akina madrid, barcelona, man u, Bayern n.k wanapotezaga game lakini kimyaa tu maisha yanaenda
 
Maneno ya kishabiki tu hayo ni ya kawaida kwenye michezo, hata timu nyingine zinaweza kutafuta naneno yao ya kuwahamasisha,sijaona shida yoyote ile,kupoteza game moja sio sababu ya kutoendelea kufanya vizuri tena
Hoja ni aina ya mpira unaochezwa. Pasi na udwambwi usambwi mwingi bila malengo na mikakati thabiti ya kupata magoli. Kucheza mpira unaovutia na kisha kufungwa ni ujinga kama ujinga mwingine. Lengo liwe kushinda.
 
Umemjibu vizuri huyo mjinga yani wabongo wanajifanya kuujua mpira lakini wakipewa timu wanazingua. Juzi nlimsikia Julio et anaishauri Simba yeye kapewa sijui timu gan kaishia kupuyanga.
 
Tatizo sio mpira carpet. Tatizo ni marefa wanao acha rafu mbaya ziendelee Kwa muda mrefu na matokeo yake kupelekea ngumi uwanjani.
Sasa hilo pira gwaride ndio utaenda kucheza kwenye mechi za kimataifa? Si timu nzima wataishia kupewa kupewa kadi za njano na hatimae nyekundu. Marefa wa kimataifa hawawezi kuvumilia huo mpira unautaka wewe.
Mpira ni sayansi na sio maguvu.
 
Mpira ni magoli, Mbumbumbu wamekalia mpira ni Mariam Biriani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…