Nadhani Simba waache ujinga wa "sijui pira biriani"

Nadhani Simba waache ujinga wa "sijui pira biriani"

Kwahiyo ninyi hamtaki kufungwa?

Yaani mkifungwa tu nongwa acha utoto basi.
Yaan hizi timu zetu za simba na yanga ni shida. Zikifungwa tu ai kutoa sare wanaanza kutafuta mchawi.

Hivi mbona akina madrid, barcelona, man u, Bayern n.k wanapotezaga game lakini kimyaa tu maisha yanaenda
 
Maneno ya kishabiki tu hayo ni ya kawaida kwenye michezo, hata timu nyingine zinaweza kutafuta naneno yao ya kuwahamasisha,sijaona shida yoyote ile,kupoteza game moja sio sababu ya kutoendelea kufanya vizuri tena
Hoja ni aina ya mpira unaochezwa. Pasi na udwambwi usambwi mwingi bila malengo na mikakati thabiti ya kupata magoli. Kucheza mpira unaovutia na kisha kufungwa ni ujinga kama ujinga mwingine. Lengo liwe kushinda.
 
Hujui mpira wewe...Kufungwa kupo tu...hata ucheze mpira wa vurugu kama walivyofanya Prison. Jiulize Prison hushinda mechi ngapi kwa msimu na mpira wao unaoshauri Simba icheze?

Eti "wamefungwa kisa mpira biliani" yaani hujui hata kwanini Simba inaitwa Lunyasi unataka kujifanya shabiki? Kila timu inafalsafa yake na husajili kocha na wachezaji kutokana na falsafa yake.

Mpira ndo ulivyo kama hutaki kufungwa kacheze Video game ili ucheze kwa mfumo wako usitupangie.
Umemjibu vizuri huyo mjinga yani wabongo wanajifanya kuujua mpira lakini wakipewa timu wanazingua. Juzi nlimsikia Julio et anaishauri Simba yeye kapewa sijui timu gan kaishia kupuyanga.
 
Mpira ni magoli.
Hii dhana ya kucheza entertaining football naona ni ya kijinga sana.Maana inategemea vitu vingi sana ili ifanikiwe. Mfano mechi ya jana na Prisons. Prisons wamecheza Mpira wa nguvu na vurugu sana.Uwanja wenyewe hauruhusu hizo pasi za rula.Kasi ya wachezaji wa Simba siyo kubwa.Upangaji wa timu na game plan mbovu.Huwezi kupata matokeo kwa jinsi hiyo.

Simba wawekeze kwenye kupata ushindi na waachane na maneno ya Haji. Kuna baadhi ya watangazaji wanasifia eti "soft touch" huu ni upuuzi mkubwa. Mpira wenyewe ni wa kiume hivyo uwekezaji wa nguvu lazima uende sambamba na akili na kipaji.

Kutokana na hii dhana na falsafa ya pira biriani imesababisha wachezaji kama Miqueuson na Morrison waache aina ya mchezo wao uliokuwa unaleta hatari sana kwa timu pinzani.Haya mambo ya chenga twawala ni ya kizamani sana
Tatizo sio mpira carpet. Tatizo ni marefa wanao acha rafu mbaya ziendelee Kwa muda mrefu na matokeo yake kupelekea ngumi uwanjani.
Sasa hilo pira gwaride ndio utaenda kucheza kwenye mechi za kimataifa? Si timu nzima wataishia kupewa kupewa kadi za njano na hatimae nyekundu. Marefa wa kimataifa hawawezi kuvumilia huo mpira unautaka wewe.
Mpira ni sayansi na sio maguvu.
 
Mpira ni magoli, Mbumbumbu wamekalia mpira ni Mariam Biriani
 
Back
Top Bottom