Jana May 20 ulitokea mshtuko baada ya akaunti nyingi za mitandao ya kijamii kudukuliwa kwa pamoja idadi kubwa ikiwa taasisi za Serikali. Watu hawa wametumia kurasa za mtandao wa X na youtube.
1. Mitandao hii miwili ya X na youtube inarusu third party app kustream. Mfano nataka kuweka tukio liwe live, naunganisha camera kwenye mifumo maarufu ya kuchakata video kama OBS na LiveU kisha naipa ruhusa OBS kupublish kwenye kurasa yangu ya mitandao ya kijamii. Hivyo nakuwa nina uwezo wa kuiweka video live kutokea kwenye OBS bila hata kuingia youtube na kuiruhusu.
Ndio maana machapisho yote yaliambatana na video.
Hizi third party apps nyingine ni changa na haziwekezi kwenye mifumo ya usalama kama ambavyo X na youtube wamewekeza, uwezekano wa kuingilia inakuwa mteremko kidogo hivyo inawezekana na njia ya kwanza iliyotumika.
Huwa haishauriwi hata kwa watumiaji wa kawaida kuruhusu third party kuwa na uwezo wa kufanya chochote au kuchukua chochote na ikilazimika basi baada ya matumizi ni muhimu kuondoa access husika
2. Kurasa nyingi zilizodukuliwa zinakaribiana sana kimahusiano, nyingi ni za Serikali ukiacha Airtel na Simba. Kwenye tasnia ya video na hii huduma ya live ziko kampuni zinafanya hii kazi ya kuchukua video na kuzirusha kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za mteja(Kwa case yetu mteja anaweza kuwa TRA, Airtel etc). Kutokana na kukaribiana huko inawezekana kwa namna moja au nyingine wameshawahi kufanya kazi na huyu mtoa huduma kila mmoja kwa wakati wake.
Ipo namna ya kumruhusu mtoa huduma aweze kurusha video kwa tukio husika pekee lakini inahitaji mwenye kurasa aweze kuingia mwenyewe na ampe link ya kurushia. Namna ya pili na inayotumika sana ni mteja kumpa access mtoa huduma na application yake access ya kuchapicha video kwenye kurasa yake, huyu mtoa huduma hubaki na access na wengi hawakumbuki kuzitoa baada ya shughuli kuisha au hawatoi kwasababu mtoa huduma anakuwa yeye anajirudia hivyo hawaoni umuhimu wa kuweka kila mara.
Yawezekana PC/device ya mtoa huduma ilifika kwenye mikono ya mtu mwenye nia ovu akafanya hili jambo au mtu huyu aliangalia namna ya kufanya akaona uchochoro ni huo.
Watanzania ikifika kwenye usalama wa kidijitali huwa tuna kauli ''Hatuna cha kuficha/kupoteza'' ila tunasahau wengine ni maadim kwenye akaunti za ofisi, wengine wanatuma picha za utupu kwenye mitandao, wengine wanasengenya mabosi zao kwenye chats. Boko moja linaweza kuondoka na kibarua, heshima na jinai ukakufata, ni muhimu kujilinda kwenye huu ulimwengu mpya.
soma Waliodukua ukurasa wa Polisi X (Twitter), wadukua ukurasa wa CCM, Airtel, Simba SC, TRA, EWURA na zingine