Nadharia ya miaka 1,000 duniani ni sawa na siku moja mbinguni si sahihi kabisa

Da'Vinci naendelea kukusoma.Unaelekea kumpinga Mungu(sio Shetani,maana kwa wengine hata Shetani ni mungu) in everything.Je wewe ni wa sinagogi la Shetani?I am just thinking loudly.
 
Da'Vinci naendelea kukusoma.Unaelekea kumpinga Mungu(sio Shetani,maana kwa wengine hata Shetani ni mungu) in everything.Je wewe ni wa sinagogi la Shetani?I am just thinking loudly.
Mimi nampinga Mungu kivipi?? Sidhani kuhoji vitu vinavyohusu Mungu ni kupinga uweza wake.

Je wewe unakubaliana kwamba Mbinguni kuna muda?? Au muda upo tu huku kwenye sayari zetu
 
Kama tu kwenye sayari zinatofautiana

Mwaka mmoja wa hapa hauwezi kuwa sawa na kwenye sayari ya jupiter au pluto sikwambii huko mbinguni!

Inawezekana bwna
Naomba msaada mtaalam kwa maswali haya madogo, kutokana na hoja zako za hapo juu:

1. Kwani mbinguni ni wapi?
2. Mungu anapatikana wapi?
3. Je yupo katika miongoni mwa Sayari hizi tunazozijua
4. Ili tupate siku, dunia hulizunguka Jua/Sun (nyota iliyo karibu zaidi na dunia). Mzunguko unapokamilika in 24hrs ndipo hufanya siku 1. Je huko aliko Mungu (kama hapa duniani hatunaye) kifaa alichopo pia hulizunguka hili jua letu?
5. Je si sahihi kusema kuwa Mungu yupo hapa duniani na kila mahali katika Ulimwengu/Universe?
 
Hii comment inafikirisha sana. Nimeipenda.

1. Yaani je zile siku zilizokuwa zinahesabiwa 1, 2 hadi 7 zilikuwa ni siku zipi hizi za dunia yetu au siku za kule kwake alipo wakati akiumbwa?

2. Je pale panaposema 'Ikawa usiku, ikawa mchana..siku 2 nk., je ilipoingia ule usiku naye akawa gizani hadi kulipopambazuka na kuwa siku mpya?

Kama aliviumbia hivi vitu akiwa huko aliko na hizo siku ni za kwake, basi naona hoja yako ya kuwa dunia na vitu vyote viliumbwa kwa muda sawa na miaka 7, 000 ya duniani na kwamba alipumzika baada ya siku hizo. Ingawa hapa pia kwenye kupumzika kama kulivyotajwa kwenye biblia kuna leta swali Jipya kuwa Je Mungu naye anachoka? Maana kuchoka ni dalili ya kuishiwa nguvu na udhaifu (binafsi naamini Mungu ni muweza wa kila kitu na hajawahi kuchoka wala kulala).

Nyaka-One
Davinci
 
Siku 7 zipi? Maana amesema siku 1 kwake ni sawa na za kwetu 1000. Sasa amehesabu siku 7, huoni hapo ni sawa na miaka 7, 000 ya huku kwetu? Maana hivyo vitu na hizo sayari alitengeneza akiwa huko (kumbuka hivi vitu huku duniani na kwengineko havikuwepo kabla ya hizo siku). Fikilia vizuri hapo.
 
Mambo Ya Rohoni Kuyafasiri Kwa Jinsi Ya Mwilini Ni Ukengeufu Na Uposhaji Wa Maandiko. Mambo Ya Rohoni Yanajulikana Kwa Jinsi Ya Rohoni Tu. Biblia Haisomwi Kama Gazeti Au Kitabu Cha Historia.
Umeamua kujiwekea ukomo wa kufikili. Sasa kama wanaoeleza kwa jinsi ya mwili wamekengeuka, Waeleze wewe basi vizuri maana wewe ni wa rohoni.
 
mzee jupiter inazunguka umbali mrefu zaidi kuliko dunia kwa orbit zao ni tofauti.
 

Sitaki kuongelea biblia kwa mifano yako hiyo kwa kuwa biblia ni kitabu kilichojaa mafundisho na maneno ya binadam na hata lugha yake ya asili haipo.

Kuhusu miaka uisemayo kwenye Qur'an imeongelewa ki aina nyingi na kipekee. Sina haja ya kuzirudia ispokuwa fahamu kuwa:

1) Qur'an ipo katika lugha yake ya asili iliyokuja nayo miaka zaidi ya 1,400 nyuma, haijabadilika na wala haitobadilika.

2) Muujiza mmoja wapo wa Qur'an ni kila inapoongelea kitu huongelea kitu hicho kilipotokea au kiongelewacho kwa misamiati (lexicons) ya sehemu na wakati husika (locution).

Kwa maana hizo, ili kuielewa aya au nukuu ya Qur'an ni lazima uielewe misamiati iliyomaanishwa kwa kila lilipoongelewa. Huwezi kuitafsiri 1ur'an neno kwa neno ikaleta maana halisi hata uitafsiri kwa Kiarabu.

Kwa hiyo miaka 1,000 au 50,000 au yoyote itajwapo kwenye Qur'an, kwanza uelewe imeongelea nini hapo Qur'an, ilikuwa inanukuu watu au mtu au onyo au amri au kisa? Na mengineyo mengi. Kama huyajuwi yote hayo hutoweza kuelewa kimekusudiwa nini ilipotajwa hiyo miaka.

Ukitaka kuelewa, weka nukuu ya aya uliyo ikusudia ili kama tunaelewa kimekusidiwa nini, tukupe darsa. Nje ya hapo tutabishana na kunukuu kijinga tu.
 
Mwenye hekima na elimu yeyote anaachana na maandiko ya kibinadam kitaka kuujua ujumbe wa Mwenye Mungu.
 
"mbinguni" ndiyo wapi mleta mada?

Maneno yako unayafanya kuwa ya Allah?

Hizo aya ulizoweka sijaona neno "mbingu" wala "mbinguni".

Naona lugha imekupiga chenga ndiyo maana umeshindwa kuelewa.
 
"mbinguni" ndiyo wapi mleta mada?

Maneno yako unayafanya kuwa ya Allah?

Hizo aya ulizoweka sijaona neno "mbingu" wala "mbinguni".

Naona lugha imekupiga chenga ndiyo maana umeshindwa kuelewa.
Kwa hiyo dada utapewa midume rijali mingap manululain
 
Panaweza kuwa na ukweli ndio maana Nabii Mussa alipokua akitoka kuonana naye anarudi ka umri kamesogea kuliko wenzie
Kwaio unataka kusema wenzake walimsubiri Kwa zaidi ya miaka elfu moja na bado akawakuta?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…