Naelekea kufilisika tena

Naelekea kufilisika tena

Annonymous

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2013
Posts
688
Reaction score
1,126
Habari wana jamvi JF

Toka nimeanza kujitegemea nimekuwa na vipindi maisha yananyooka. Yani kila unalofanya jah analibless . Ukitupa wavu sokoni kazima uvune pesa za kutosha. Sasa huwa naenda weeee kisha badae hela zile zinarudi zilikotoka yaani biashara inakuwa ngumu, ni kutumia tuuu na wakati mwingine ukituma hela kwa mlengwa kwa matumizi fulani italiwa.

Mara chuma ulete wkt mwingine kuibiwa au kupoteza. Yaani ilimladi pesa zipukutike tu nirudi masikini nianze moja tena upya kabisa hivyo. Sasa hapa katikati nilipata hela nikaenda nikajenga vyumba kadhaa mkoani nikarudi nikasongesha mambo super nmenunua pkpk na kiwanja mambo maswanu.

Sasa kumekucha pikipiki inasumbua haiishi matatizo, kazini ni hasara tu, kitega uchumi changu wateja hakuna nna madeni na naona kabisa mwezi ujao nikitoboa salama ni bahati maana kuna kila sababu ya kurudisha mpira kwa kipa tena.

Wakuu nyie huwa mnafanyaje mambo yananyooka mstari mnyoofu miaka na miaka
 
“Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake.”
— Mhubiri 7:14 (Biblia Takatifu)
 
Maisha ndivyo yalivyo. Kuna kukosa, kuna kupata, kuna kufanikiwa, kuna kushindwa, kuna kuteremka, kuna kupanda. Hivyo unatakiwa kupiga moyo konde.

Usiangalie ulipoanguka! Angalia pale ulipo jikwaa.
 
Habari wana jamvi JF

Toka nimeanza kujitegemea nimekuwa na vipindi maisha yananyooka. Yani kila unalofanya jah analibless . Ukitupa wavu sokoni kazima uvune pesa za kutosha. Sasa huwa naenda weeee kisha badae hela zile zinarudi zilikotoka yaani biashara inakuwa ngumu, ni kutumia tuuu na wakati mwingine ukituma hela kwa mlengwa kwa matumizi fulani italiwa.

Mara chuma ulete wkt mwingine kuibiwa au kupoteza. Yaani ilimladi pesa zipukutike tu nirudi masikini nianze moja tena upya kabisa hivyo. Sasa hapa katikati nilipata hela nikaenda nikajenga vyumba kadhaa mkoani nikarudi nikasongesha mambo super nmenunua pkpk na kiwanja mambo maswanu.

Sasa kumekucha pikipiki inasumbua haiishi matatizo, kazini ni hasara tu, kitega uchumi changu wateja hakuna nna madeni na naona kabisa mwezi ujao nikitoboa salama ni bahati maana kuna kila sababu ya kurudisha mpira kwa kipa tena.

Wakuu nyie huwa mnafanyaje mambo yananyooka mstari mnyoofu miaka na miaka
Vyumba ulivyojenga mkoani na kiwanja, ni vya makazi au biashara?
Pikipiki ni kwa matumizi yako au biashara?
Kila ufanyacho, angalia fursa - eneo na muingiliano wa watu (wateja), soko - uhitaji wa hiyo huduma/bidhaa hapo ulipoona fursa. Na jitangaze - uwekezaji uwe wa kiwango cha juu, mteja aridhike, afurahie na kujisikia kufaidika na huduma yako na asione kama anakusaidia wewe. Wafuate na uwatafute wateja wasiojua uwepo wa huduma yako.
Usiache kujiwekea akiba. Kila uvunacho, weka akiba kiasi baada ya matumizi ya lazima. Hii inasaidia inapotokea fursa fulani, na wewe una pesa ya akiba, basi kama fursa inakufaa, unawekeza zaidi, na hivyo kujiletea maendeleo.

Kwa ujumla biashara ni ngumu na kwa Tz ni ngumu zaidi, kwani uchumi ni dhaifu, ukiongeza na rushwa, ubadhirifu na wizi, biashara yoyote inakuwa bahati nasibu.
Pambana unavyoweza,
 
Back
Top Bottom