Naelekea kupoteza mafao yangu, ushauri wenu Wanasheria

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2018
Posts
456
Reaction score
833
Habari ndugu zangu,

Niende Moja kwa moja kwenye tatizo langu.

1. Mwaka 2017-2019 niliajiriwa sehemu nikawa nalipwa ujira wangu, nilikuja kuachana nao na kujiunga na taasisi nyingine, Hawa maboss wangu waliniahidi kiasi Fulani Cha fedha wanapeleka NSSF lakini hawakuwa wakifanya hivyo, na kibaya zaidi mikataba walikua hawatupi wanasain znabaki kwao, baada ya kumalizana nao nimeenda NSSF wanadai malalamiko yangu nimechelewa kuyapeleka nilipaswa kuangalia kipindi nipo kazini kama mafao yangu yalikua yakiwekwa.. Tena najibiwa kwa hasira sana, na kuambiwa siwezi kusaidiwa Tena kwani hiyo taasisi inamilikiwa na mtu mwingine kwa Sasa.

2. 2019 - 2021 nilijunga na taasisi nyingine, hii taasisi ilikua na majanga sana walikua wanalimbikiza mishahara ila walinipa mkataba, siku naachana nao mkurugenzi alikuja akasema kama hamridhiki na uendeshaji sahivi nimeyumba njoo ofisini sain na uondoke, Mimi nilienda kuacha kazi, nikiwa nawadai kama 2M hivi, walinipa kimafungu mpaka ikabaki 400'000 ambayo mpaka kesho naambiwa tuu tutakupa kuwa na subira, Sasa NSSF hakuna kitu walikua wakipeleka badala yake ahadi zilikua nyingi tunapeleka tunapeleka lakn hakuna lolote, wahusika wa NSSF majibu ni Yale Yale, kwamba taasisi hiyo eti ni wasumbufu sana, hivyo ni vigumu kuwadai... Aisee nimesikitika sana.

Miaka yote hio nafuatilia lkn hamna lolote, vithibitisho vyote ninavyo including Salary slip za benki... Kwa kazi zote mbili!

Nifanye nini ndg zangu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…