TUKANA UONE
JF-Expert Member
- Jan 3, 2018
- 2,345
- 6,970
Huwa ninapokuwa napata muda na nimepumzika mara nyingi huwa napenda kufuatilia kipindi kimoja kinaitwa AIRPORT SECURITY ambacho kinapatikana katika channel ya NATIONAL GEOGRAPHIC kutoka king'amuzi Cha Dstv
Kipindi hiki mara nyingi kinaangazia masuala ya usalama katika Viwanja tofauti tofauti vya ndege huko duniani
Leo nitaongelea matukio mawili ambayo yamefanya nikaandika huu Uzi
AIRPORT SECURITY : RIO de JANEIRO
Kuna jamaa walikuwa 6(Washikaji 4 na mademu 2) kutoka nchini Ghana walijilipua na kufika Airport ya hapo Rio de Janeiro nchini Brazil wakajifanya mabubu 😁
Maafisa wa usalama wamekomaa kweli kuongea na Washikaji ila jamaa wakawa hawafungui midomo (Bila shaka nadhani walikubaliana),baada ya maafisa kuwakomalia na kuwaambia kama hawataki kuongea wanaenda kuwarudisha walikotoka,ndipo jamaa wakaanza Lia Kwa nguvu Ile ya kiafrika hadi kugalagala chini 😁😁,Kuna mmoja huyo yeye akajifanya mlemavu hawezi Kutembea,ilifika sehemu hadi maafisa wakawa wanacheka 😁!
Jamaa wakawa wanasema "Ghana killing.........Ghana killing ......Ghana killing,we are not go back to Ghana,it's better you Brazilian Police kill us but we are not go back to Ghana"😂😂😂
Daaaah maisha haya,nikawa najiuliza mbona Brazil yenyewe pia siyo kuzuri sana kama Europe!
Ok but jamaa waliwekwa kwenye kundi la watu ambao ni wahamiaji.
AIRPORT SECURITY : ROME (ITALY)
Leo pia katika kutazama kipindi nikaona Kuna watu wawili (Mwanamke na Mwanaume) wakiwa wanakaguliwa Pasipoti zao na kuulizwa maswali kadhaa na watu wa customs pamoja na maafisa usalama!
Yule jamaa na demu baada ya kukaguliwa walionekana wako sawa kwenye documents zao ila maafisa walipata shaka baada ya kuulizwa hapo Italy wamekuja kufanya ishu gani,Jamaa ambaye aliweza kuongea kiingereza kidogo alisema wameenda nchini Italy kupumzika na Kutembea kama watalii,nadhani maafisa hawakuridhika na maelezo hayo,ikabidi demu na mshikaji wapelekwe huko vyumba vya ukaguzi na kila mmoja akaingizwa kwenye chumba chake na kuanza kuhojiwa kivyake !
Baada ya kila mtu kuhojiwa kimpango wake,demu akasema mshikaji ni shemeji yake,na jamaa akasema demu ni mke wake kabisa wa ndoa!😁
Baada ya kubanwa na kukaziwa macho na maafisa,demu akasema mshikaji ni rafiki yake na mshikaji akasema demu ni Dada yake 😁
Nikawa najiuliza Hawa watu mpaka wanafanikiwa kupata visa ya Italy Ina maana hawakujua kunaweza kutokea maswali kama hayo?
Kwanini wasingekubaliana wakiwa bado AFRIKA kwamba wakiulizwa wasemeje?
Jamaa nikaona wameambiwa wanarudishwa walikotoka 😁
By the way ni kipindi ambacho huwa kinafundisha sana maana wanakamatwa watu kibao na drugs dealer ndo huwa kama wote!