Naenda Arusha kununua Gitaa la Garatoni. Nijuzeni ni vitu gani vya kuzingatia

Naenda Arusha kununua Gitaa la Garatoni. Nijuzeni ni vitu gani vya kuzingatia

DeMostAdmired

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Posts
1,579
Reaction score
3,798
Wakuu habari zenu?

Leo nitatoka mkoa jirani nilipo nitasogea Arusha kuchukua GITAA la garatoni ili niweze kuanza rasmi mafunzo ya gitaa. Nina ndoto toka zamani kuja kuwa mpiga vyombo vya muziki (mniombee niitimize).

Mwalimu nishampata lakini ni mzee yeye anapiga kwenye band moja hapa mjini sasa kanishauri nikanunue gitaa la garatoni kwasabab gitaa yeye hana anatumia electric ambalo ni la ofisini.

Naombeni mnijuze gitaa lipi ni zuri, vitu gani vya kuzingatia katika kufanya manunuzi ya kifaa hiki hata na picha mkiweka itakuwa poa zaidi na pia mnijuze accessories zake ili nisije nikanyimwa haki zangu za msingi kwenye package ya chombo hicho.

Ahsanteni!
 
Nadhani mtu sahihi angekuwa huyo mwalimu wako aliyekuambia ununue hilo gitaa, au nae hajui aina ya gitaa zuri? Ama umetaka kupata michango zaidi ya wadau wa jukwaani? kila kheri mkuu ukafanikiwe ndoto zako.
 
Mzee ni mzee kaka nahitaj mawazo ya kisasa, yeye atakwambia kuhusu magitaa ya kizaman
 
Nunua kwanza zeze kama la TID.

Au kama kweli umedhamiria unataka gitaa zuri nunua Martin D28 bei yake ni million 8 na kidogo, achana na hayo ya laki 3
 
Back
Top Bottom