ndugu,
samahani nilitoka kidogo.
nawashukuru sana wote waliochangia thread yangu na kwa hakika nimenufaika sana na mawazo yenu wote. Shukrani za pekee kwa wote walioniunga mkono na kunitia moyo. Safari ni ndefu na ita ni vigumu, lakini nafarijika ninapoona kuwa ushindi ni dhahiri upande wangu.
Nikiri kwamba changamoto ya kuwaania ubunge ndani ya ccm ni kubwa sana, yako mambo ya ufisadi, wizi wa kura, kuhadaa wapiga kura, nk. Hayo yamo ndani ya chama chochote cha siasa japo ukubwa wa tatizo ni tofauti toka chama kimoja hadi ingine.
Kuhusu ccm skubaliani kuwa wote ccm ni mafisadi na naweka wazi uwa mimi si fisadi wala sitafuti ubunge niwe fisadi. Nikifanikisha azma yangu, mtakubaliana nami kuwa kwa mara ya kwanza vita ya kweli dhidi ya ufisadi itapganwa na mbunge wa ccm bila shaka nitakuwa mimi, tuombe Mungu, tutafika
Matajiri wa kutisha ndani ya ccm wapo, sikatai lain si wengi kama inavyoaminka. Kuna watu kanitajia majina ya panda, wasira na mkono. Wote nawafahamu na nawaheshimu sana, lakini siogopi kupambana nao kisiasa. Mtaji wangu mkubwa ni nguvu ya wananchi na naamini naweza kushinda hata nikipambanishwa na nani na mwenye shilingi ngapi.
heshima ya pekee kwa mku next level kwa uchambuzi wake makini. Ni kweli kuwa kwa mujibu wa uchambuzi wake na viambatanisho alivyowasilisha, sifai hata kidogo kwa wadhifa ninaoutafuta kwani matendo yale ni kinyume cha maadili. Naomba niwarudishe nyuma kidogo.
Toka siku ya kwanza najisajli JF nilisema kuwa kama jna langu lilivyo ndivo ilivyo dhamira yangu. Nivyo ndio maana sijitambulishi kuwa nagombea ubunge, bali natoa taarifa kuwa katika siku za karibuni sitaonekana mara nyingi hapa JF na wapendwa msijiulize kulikoni.
Siku za mwanzo hapa JF nilikuwa naleta visa vingi sana vya matatizo ya ndoa na namna nilivyojaribu kuvisuluhisha. Katika visa vile sikuwahi kuweka hadharani majina ya wahusika kwa malengo maalum ambayo kila mtu mstaarabu atakubaliana nami kuhifadhi majina yao. Lengo halikuwa kudanganya, bali kulinda heshima na madili.
Hivyo kuna wakati mtu anasema ama anakaa kimya au anatumia majina bandia kwa lengo la kulinda kitu ama kuelewesha vizuri kitu Fulani. Na ndivyo nilivyofanya mimi. Na ndivyo wafanyavyo na wanJF wengine. Hivyo post aliyotumia next level inaonekana kama ni mimi haswa, bali ukweli ni kwama nilihifadhi jina halisi la mhusika na nikaisimilia kama ni mimi wenyewe kwa lengo la kufikisha ujumbe uliokusudiwa na ambao naamini ulfika. Kukereka walikokereka wachangiaji hapa JF ni kiashiria kingine kuwa ujumbe uliokusudiwa ulifika kikamilifu. Labda kosa la kukiri hapa ni kuwa sikusema tangu mwanzo kuwa si mimi bali nimetumia mtindo wa uandishi kama vile mimi ndiye. Hapo naweza kusema smahani kwa kuwapotosha wale niliowaptosha. Kweli hata mimi napinga sana matendo ya kifataki katika jamii yetu.
Tuendelee kukabiliana na matendo ya aina hii bila kuchoka na naamini ushindi ni wetu.