'Naenda Kusema' ilivyosababisha Aslay achezee kichapo

'Naenda Kusema' ilivyosababisha Aslay achezee kichapo

sangujoseph

Senior Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
164
Reaction score
183
By Sangu Joseph

Leo nimekikumbuka kisa kilichonichekesha baada ya kukutana na wimbo wa Aslay Rudi Darasani hasa kile kipande ambacho video vixen anatamba kwamba alienda kuwaona wageni, Akiwa amevaa short pensi, na Tabu Mtingita ambaye ndiye kungwi aliyetoa boko anamwambia unajikuta Beyonce.

Kilichonifanya nikumbuke mimi nilibahatika kusoma na Star Aslay Isihaka pale Tandika Sekondari japo nilimpita darasa moja.

Wakati ngoma yake ya Naenda Kusema kwa Mama (2011) inatamba, interview kila media kiufupi kama zote, siku moja alienda kwenye kituo cha redio cha Clouds FM. Sasa wakati anaulizwa maswali na Dahuu alisema kwamba siku hizi shule hachapwi wala viongozi wa shule hawampi fagio akafagie.

Basi Jumatatu yake baada ya kufika shule akakutana na kiongozi (Kiranja kauzu) mmoja alikua anaitwa Theodory Mwingira; alisikia yale mahojiano, basi jamaa hiyo siku alichelewa kufika yule mshikaji akampa adhabu ya kufagia, kufyeka na kuzoa taka kwenye eneo lenye nyasi nyingi.

Kutokana na u-star aliokuwa nao kiukweli ilikuwa ngumu sana kulifanya hata kama ningekua mimi. Aslay akawa anaingilia huku anatokea huku, kiufupi alikuwa analinda brand, basi yule kiranja kauzu akaenda kusema kwa ticha kauzu alikua anaitwa Likalambile, anafundisha Mathematics hatari na kama mnavyojua Walimu wa Mathe wanakuaga wakali sana. Basi Aslay aliitwa na ticha alipigwa bakora mpaka alitoroka shule kwa bakora za yule mwalimu.

Ikawa bonge moja la stori shule nzima Aslay kachezea kichapo tena yule Mwalimu alimpiga akimwambia 'Nenda kaseme kwa Mama'

Ila ambacho nilijifunza, shule zetu hazina utaalamu wa kulea watoto wenye vipaji ila wanauwezo wa kulea watoto wenye akili za darasani. Nadhani kuna haja shule zetu kuwa-treat sawa watoto wenye vipaji na wenye akili za darasani.

#KijanaMzalendo #IloveTZ Nicheki Instagram na Twitter na Facebook sangujoseph Kwa makala na uchambuzi ninaoufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimekumbuka mbali lol sir wa mathe nikiwa o,Lev alinichapa fimbo had nikahisi kupooza kisa nilipata alama zisizomridhisha wakati me nilikuwa 1 ya tegemeo lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeanza vzr umemaliza vby haha
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimekumbuka mbali lol sir wa mathe nikiwa o,Lev alinichapa fimbo had nikahisi kupooza kisa nilipata alama zisizomridhisha wakati me nilikuwa 1 ya tegemeo lake.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo shule aliyosoma Aslay kuna madam anaitwa Joyce Killa. Unamkumbuka?
 
Wabongo ukiwazid wanaona kama unajiona , wanatafuta namna ya kukuweka down
 
  • Thanks
Reactions: THT
Back
Top Bottom