Nafanya biashara ya nguo za kike -Nyegezi Mwanza, Wapi kuna soko zuri la nguo?

Nafanya biashara ya nguo za kike -Nyegezi Mwanza, Wapi kuna soko zuri la nguo?

chambimagaka

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2017
Posts
288
Reaction score
338
Habari wanaJF, katika hali ya kujishughulisha ili mkono uende kinywani, niliamua kufanya biashara ya nguo za akina Dada Na mama kwa ujumla! Natamani biashara yangu itanuke Na ikue haswa!!
Nashukuru mungu biashara inaenda vizur!

Ila sasa kinachonisibu ni sehemu IPI nzuri yenye bei ya nzuri ambapo naweza kwenda kununua mzigo wa jumlajumla Na mm nije niuze rejreja? Kwa maana kwa sasa nachukulia maduka ya APA APA Mwanza, Na natamani sasa niende mbali kidgo iwe DSM,Kampala au Nairobi, lkn angalau nipate unafuu tu!

Naombeni ushauri wenu Na uzoefu wadau!

Karibuni sana!
 
wauza nguo mwanza wengi wanafuata mizigo kampala.. na kampala to dar ni karibu na less costly kulinganisha na mwanz to dar.
 
Kama mtaji wako aujakuwa usilazimishe kwenda mbali kuchukua hizo nguo ww endelea kuchukua hapa mwanza ila kama mtaji wako umekuwa kutana na watu wanaenda kampala wakuelekeze nguo za kampala ni bei rahisi sana
 
Jikite mikoa ambayo inachangamoto au iko mbali na majiji makubwa huko kuna uhaba wa nguo za kike na utauza kwa bei kubwa sana.
 
Back
Top Bottom