SoC03 Nafasi na utambuzi wa nafasi

SoC03 Nafasi na utambuzi wa nafasi

Stories of Change - 2023 Competition

Machilllo

New Member
Joined
Jun 4, 2023
Posts
2
Reaction score
1
Katika Maisha tunajifunza kuwa, kila mtu haijalishi ni umri, rika, jinsia, ama uwezo alio nao huwa una msukumo katika kufanya jambo Fulani. Jambo hilo linaweza kuwa kwa ajili yake, ama kwa ajili ya jamaa wanao mzunguka. Kwa mfano tunapokuwa Watoto mara nyingi tunakuwa na akili ya kufanya vitu mbalimbali kwa kuwasaidia ama kutokuwasaidia watu wengine kutokana na namna tunavyo ambatana nao, huwa tunajali sana watu wa nyumbani ukilinganisha na watu wa nje kwa sababu ya nafasi tuliyowapa watu wa nyumbani na vile ambavyo huwa tunaona wakitusaidia, wakitupenda na kuwepo Pamoja nasi wakati wote ambao tupo nao, kwa ufupi huwa tunawasaidia na sisi kwa sababu nao wanatusaidia. Vivyo hivyo kadiri tunapozidi kukua vitu kama mazingira, na jamii inayotuzunguka kwa ujumla huwa vinakuwa na msukumo mkubwa wa namna gani tunapaswa kuishi na kuingiliana na watu wengine. Tunajifunza kwamba kuna watu wema na kuna watu wabaya wote tunapaswa kuishi nao haijalishi ni kwa uzuri ama ni kwa ubaya, “ni vile TU, tunavyoona namna wanavyoishi na sisi”.

Nataka kusema kwamba “tunakuwa tukitoa muda wetu mwingi kwa watu wale ambao tunapata amani tukiwa nao”. Kutokea hapo tunakuja kugundua kwamba katika jamii ni nafasi gani inafaa kwetu na ni kwa muda gani tunatakiwa kuishi katika hiyo nafasi. Tunapojua hali tupo na watu ambao sio salama kwetu huwa tunachukua nafasi ya kujihami na kujilinda ili maneno yao ama vitendo vyao visiweze kutudhuru na vilevile tukiwa na watu ambao ni muhimu kwetu na tunakuwa na amani tukiwa nao tunabadili nafasi ya awali na kuchukua nafasi nyingine ambayo tunakuwa na uwezo wa kuongea jambo lolote kwa kujiamini, na kuwa tayari kujifunza kutoka kwao kwasababu tu tayari tunajua kutoka kwao huwa hatutoki mikono mitupu “kuna vitu vingi huwa tunajifunza kutoka kwao. Hasa wale ambao tayari wanakuwa wametuzidi katika eneo Fulani ambalo tunatamani Zaidi kulijua”. NI MAISHA.

Hivyo, tu(na)jifunza kuwa ukuaji wetu mara nyingi huwa unaathiriwa na maisha ambayo huwa tunakuwa tumekulia.

Nitatolea mifano kutoka kwa viongozi wetu wawili wakubwa kutoka barani Afrika; Mwl Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa ni raisi wa kwanza wa Tanzania na ni Baba wa Taifa la Tanzania na kutoka kwa Mhe. Nelson Mandela aliyekuwa ni kiongozi wa wapingaji wa serikali ya kibaguzi kutoka Afrika ya kusini. NI NINI BASI TUNAJIFUNZA KUTOKA KWAO?

Tuanze na Mwl. Julius K. Nyerere.
ANP-795192.jpg

Picha ya Mwl. Julius Nyerere: ANP
Mwalimu Julius Nyerere tukiongelea kwa suala la ukuaji na mazingira aliyokulia tunapata picha kwa namna moja ama nyingine alijengwa katika misingi ya kiuongozi, kuanzia alipokuwa mdogo hata pale alipopata nafasi ya kusoma katika vyuo vya kikoloni wakati huo. Hii ina maanisha nini? kusoma, ucha Mungu na kutambua nafasi ni mambo makuu ambayo yanamsaidia mtu kuweza kusimama vyema na hata kutambua nafasi yake katika Maisha yake husika na hata kwa wengine.

Kwenye kusoma tunakutana na watu wengi ambao wanatufunza mambo mengi mazuri kwa mabaya (uchaguzi unakuwa ni kwetu kutambua ni wapi kutakuwa sahihi Zaidi kwetu..!), Ucha Mungu Pamoja na ibada kunampa mtu kuwa na uwezo Zaidi wa kupambanua mambo na hasa kwa kufanya namna yeyote ile kuyafanya yaweze kuleta majibu yenye matokeo chanya kwetu na kwa wengine, kutambua nafasi napo kunakuja baada ya mtu kujua SAWA nimechagua upande A ama upande B baada ya kupata maarifa (kwa kusoma kuliko rasmi ama kusiko rasmi) na baada ya kupata mafundisho ya hekima kutoka katika ibada (nikijumuisha mambo yote mazuri tunayojifunza kutoka katika ibada na sio DINI). Mwalimu Nyerere mpaka leo amekuwa kiongozi bora sio tu kwasababu alipigana na kulipa Taifa letu uhuru lakini pia aliijua nafasi yake, akasimama kwenye nafasi yake na aliwajibika kwa nafasi yake kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla. “kibaya chajitembeza na kizuri chajiuza” …. namaanisha kujua nafasi yako na kuwajibika katika nafasi yako ni moja ya ngao kubwa na muhimu kwako na kwa jamii pia.

Vipi kwa Nelson Mandela?
mandela.jpg

Picha ya Nelson Mandela: UNESCO
Nelson Mandela kama viongozi wengine wengi katika nchi zetu za kiafrika tunasimuliwa kwamba alikulia katika mazingira ya kawaida na kubahatika kusoma wakati huo. Katika kipindi chake tunaona kuwa Mandela alibahatika kuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi, alipata nafasi ya kukutana na watu mbalimbali wakati yupo shuleni si kwa ngazi ya chuo tu lakini hata katika ngazi ya serikali ya juu na jamii yake pia. Licha ya kubahatika kusoma, Nelson Mandela tunaona amekuwa akishuhudia unyanyasaji uliokuwa ukifanywa na serikali ya kibaguzi ya kikoloni wakati huo na jamii yake ikiwa ndio walengwa wakuu kabisa wa unyanyasaji huo. Jambo hili lilimpa hamasa ya kutaka kufanya kitu kwa ajili ya jamii yake na ni kwasababu nafasi aliyokuwa nayo ilikuwa ni ya juu ukilinganisha na watu wengine wa jamii yake.

Jamii imempa uwezo wa kutambua nafasi yake kama mtetezi, shule ilimpa uwezo wa kuvumbua Zaidi uwezo aliokuwa nao hasa kutokana na umahili wake kama mwanasheria msomi na pia wanafunzi wenzake walimpa uwezo wa kuzidi kuona kuwa anastahili kuongozi kwasababu ya kumpenda kwao, na kuonesha ushirikiano kwao katika wakati wa uongozi wake na hasa pale alipoanzisha harakati za kumkomboa mtu mweusi kutoka katika ubaguzi. Tunajifunza nini...? NAFASI...! hayo yote kuanzia kwenye mazingira aliyokulia mpaka shule alipokuwa akisoma vilikuwa ni vitu vilivyokuwa vikimpa uwezo wa kupambanua nafasi yake hasa kwa ajili ya jamii yake.

Uwajibikaji unakuja baada ya mtu kutambua nafasi yake, YEYE NI NANI, KWANINI NI YEYE, na KWANINI NI WAKATI HUO? Hatuwezi kuwa wawajibikaji kwa vitu tusivyovitambua na kuona umuhimu wake kwetu na ni vivyo hivyo hata kwa uongozi. Tunagombania uongozi kwasababu tumeona kuwepo kwa mapungufu katika maeneo Fulani ambayo kwa namna tulivyokua, tulivyojifunza, uzoefu tulioupata na kwa namna tunavyojiamini tunaweza kutatua mambo kumetusaidia kutambua nafasi zetu na hasa kwa faida ya jamii zetu zinazotuzunguka.

Hivyo, Mazingira, Watu wanaotuzunguka, Mahali tunakopita na namna tunavyochagua kujifunza bila kusahau Sala ni mambo yanayotusaidia kujua NAFASI zetu na kuwa wawajibikaji na viongozi bora.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom