Nafasi ya biashara ya juice ya miwa Kariakoo

Mamavivan

Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
10
Reaction score
3
Habari, nataka kuanzisha biashara ya juice ya Miwa kariakoo sasa Sijajua jinsi ya kupata sehemu ndogo tu iliyochangamka kwa ajili ya kuweka mashine na watu kusimana.

Pia vitu muhimu vya kuwa navyo ukitoa mashine na glass. Na mbinu za kupata wateja.

Naomba msaada kwa wenye uzoefu
 
Njoo mbande kisewe sokoni. Utanishkuru badae
 
Niliwahi kuuza duka kariakoo miaka ya 2020, nilijionea dogo janja mmoja alie kua mbele ya duka nililo kua nauza mimi akipiga pesa ndefu sana.
 
Kama una mashine tayari
Jitahidi kuwa msafi , vaa vazi la kuonesha unatoa huduma ya kitu cha kula ili usisumbuane na akina bwana afya.

Jitahidi kuchanganya tangawizi na ndimu katika hiyo juisi yako ili kuleta radha nzuri.

Jaribu kuwa na mawasiliano na watu wa kukuletea mabarafu ili uipoze vizuri na wale Waha wanaoleta miwa .

Jiepushe na kununua miwa masokoni , nunua direct kutoka kwa Waha wale wanaendesha maguta .

Namba zao utazipata kutoka kwa wauzaji wa juisi hapo kariakoo .
Hayo mabarafu jitahidi ununue kwa wale mabibi ambao ni wahindi uko kariakoo maana mabarafu yao yanakaa muda mrefu kidogo .

Ndugu kupata sehemu ya kufanya hiyo biashara ni changamoto sana.

Nakutuma mnazi mmoja , njia panda ya kwanza kabla ya kufika njia panda ya kwenda hapo Lumumba , wanauza magodoro hivyo ulizia kuna nafasi paliwahi kuwa.na mashine japo kwasasa haipo tena.

Ili usipotee ulizia ilipo benki ya CRDB ukiipata songa mbele kuelekea hapo njia panda.ni hapo hapo ulizia palipkuwa na mashine ya kukamua juisi ya miwa.

Natanguliza shukrani [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo wapi huko?
Mbande kisewe ipo karibu na msongo la kupita mbagala. Kuna soko kubwa Sana kama lile la stereo Temeke. Kuna biashara nzuri Sana kwenye lile soko. Limashika nafas ya pili Kwa wilaya ya Temeke kimapato. Hat hivyo sijaona mtu kuleta hamshahamsha za juis ya Miwa pale. Fanya kweli upige pesa mama Ivan
 

Asante sana, Mungu akubariki
 

Asante sana
 
Nami nasubiri michango na kama kuna mtu ana mashine ya umeme Used ya bei chee nae aje hapa anaione nimuungishe
 
Sema mkuu umempea bila choyo ushauri mujarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…