Kama una mashine tayari
Jitahidi kuwa msafi , vaa vazi la kuonesha unatoa huduma ya kitu cha kula ili usisumbuane na akina bwana afya.
Jitahidi kuchanganya tangawizi na ndimu katika hiyo juisi yako ili kuleta radha nzuri.
Jaribu kuwa na mawasiliano na watu wa kukuletea mabarafu ili uipoze vizuri na wale Waha wanaoleta miwa .
Jiepushe na kununua miwa masokoni , nunua direct kutoka kwa Waha wale wanaendesha maguta .
Namba zao utazipata kutoka kwa wauzaji wa juisi hapo kariakoo .
Hayo mabarafu jitahidi ununue kwa wale mabibi ambao ni wahindi uko kariakoo maana mabarafu yao yanakaa muda mrefu kidogo .
Ndugu kupata sehemu ya kufanya hiyo biashara ni changamoto sana.
Nakutuma mnazi mmoja , njia panda ya kwanza kabla ya kufika njia panda ya kwenda hapo Lumumba , wanauza magodoro hivyo ulizia kuna nafasi paliwahi kuwa.na mashine japo kwasasa haipo tena.
Ili usipotee ulizia ilipo benki ya CRDB ukiipata songa mbele kuelekea hapo njia panda.ni hapo hapo ulizia palipkuwa na mashine ya kukamua juisi ya miwa.
Natanguliza shukrani [emoji120]
Sent using
Jamii Forums mobile app