SoC01 Nafasi ya Jamii Forums katika jamii yetu ya Tanzania

SoC01 Nafasi ya Jamii Forums katika jamii yetu ya Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Jaffotz

New Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
1
Reaction score
1
Katika Taifa lolote lile lililo huru si ajabu kuona majukwaa mbalimbali yakishiriki katika mijadala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuibua hoja nzito na nyingi juu ya Taifa letu la Tanzania licha ya kwamba Kuna wakati inapigwa vita.

Kama ambayo hakuna binadamu ajuaye ni Nani aliweka maji kwenye nazi, basi ndivyo ambavyo watu wengi wanashindwa kuelewa malengo na madhumuni ya Jamii Forum.

IMG_20210708_210129_124.jpg

Kwangu Mimi ninaiona zaidi ya jukwaa lenye kuibua hoja nzito ambazo kwa upana wake zinagusa moja kwa moja mstakabali wa Taifa letu.

Ni wakati Sasa wa kukubali kuwa tunahitaji majukwaa mengi na yenye kuheshimiwa ndani ya Nchi yetu ili kuibua ari ya ujifunzaji na ubobevu katika masuala mbalimbali yanayogusa maslahi ya Watanzania.

Jamii Forums itaendelea kuwa kioo na mwanga wa jamii kwani ufanisi wake siyo wa kusuasua. Uongozi wake uko imara na wanachama wake wako imara.

Jicho langu la mbali linaniambia kuwa endapo tutakuwa na sheria zisizo kandamizi kwa Taifa hili basi mawazo chanya ya wananchi yataheshimiwa na kupewa heshima yake ili tuweze kulivusha Taifa letu kwenda mbali zaidi. Ukitaka kubadili historia basi hauna budi kuanza na mizizi ya tatizo husika ili uweze kung'oa tatizo lote.

Tuendelee kushikamana na kuwa na kauli ya pamoja kuwa lengo letu ni kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu huku tukizingatia kanuni na sheria za Nchi yetu ya Tanzania.

Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama aliwahi kusema "SAUTI YAKO INAWEZA KUBADILI DUNIA NZIMA". Tuendelee kupaza sauti zetu kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Kazi iendelee.
Ahsante.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom