Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Utakubaliana na mimi kuwa CCM inayumba sana kwa sasa kutokana na nafasi ya katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo taifa. Kila aliyeshika hiyo nafasi, kama hakupwaya basi aliishia kuwagawa wanaCCM katika makundi ya kuwania urais ama kutengeneza chuki dhidi ya wananchi.
Tatizo lilianza kuonekana zaidi ya miaka 20 iliyopita, wakati huo nafasi hiyo ikishikiriwa na Ramadhani Omary Mapuri tena akiwa na kofia mbili, moja ikiwa ni waziri wa mambo ya ndani.
Tangu Mama Samia aingie madarakani miaka mitatu iliyopita, watu wanne wamepita kwenye hiyo nafasi bila kuleta mafanikio. Kuanzia Pole Pole mpaka Makonda, kote bila bila.
Hiyo nafasi na hicho kitengo kimebakia kuwa eneo la kupika majungu, kuropoka, kutengeneza makundi, uzushi, fitina na Propaganda.
Nadhani huu ni muda muafaka zaidi wa kuamua kukifuta kabisa ili mambo mengine katika CCM na taifa yaweze kwenda vyema.