. . . kwenye conflict kati ya mke na ndugu wa mume.
Kwanza nianze kwa kuuliza. .
Hivi kwa nini ndugu wa upande wa mume (mawifi, mashemeji, mama mkwe) ndio hua wanaonekana kusababisha matatizo zaidi kwa wanandoa kuliko ndugu wa mke? Hii inasababishwa na nini?
Hili linaweza kuwa kweli au si kweli, kutegemea na jamii unayoongelea. Kuna jamii ambazo mwanamme na mwanamke "wanaoana" (kila mmoja anamuoa mwenzake) na kuna jamii ambazo mwanamme anamuoa mwanamke (kama jamii nyingi za kiafrika) na kuna jamii chache sana ambazo mke anaoa.
Nafikiri katika context yako unaongelea zaidi jamii zetu za kiafrika nyingi ambazo mume "anamuoa" mwanamke.
Kwanza mpaka hapo ushapata sehemu ya jibu. Ndoa imejengwa kwa msingi wa "mume kumuoa mwanamke". Kwa hiyo traditionally inakuwa kama familia ya mwanamme "imemchukua" mwanamke kutoka kwao. Kuna tamaduni nyingine hata kwenye harusi kaka na dada wa mume humpongeza kwa "kutuolea". Na hata mume akifa mdogo wake anaweza kumrithi mke (moja ya sababu za maambukizo ya Ukimwi).
Mfumodume huu mara nyingi humuangalia mwanamke kama chombo/ kitu, ndiyo maana analipiwa hata mahari. Na familia nyingine hufikia hata kudai mahari kama ndoa itavunjika.
Nikirudi kwenye nilichokusudia kuandika, juzi nilikua naongea na mtu maswala ya ndoa including mahusiano kati ya mke na ndugu wa mume yanavyoweza kufanya ndoa iwe chungu ikiwa hakutakua na maelewano kati yao. Mwenyewe aliniambia kwamba "matatizo yanayosababishwa na ndugu wa mume yanatokana na mume kutokua MSIMAMO pia SAUTI mbele ya familia yake."
Hili lina ukweli kiasi fulani. Lakini mimi nataka niliangalie kwa upana zaidi. Tatizo la msingi ni mila na tamaduni zilizopitwa na wakati ambazo zinachangia wanawake kuwa tegemezi na kuendeleza dhana ya mwanamke kuwa kama mali. Kwa mfano, habari nzima ya kutoa mahari inachangia kumfanya mwanamke awe kama mali "inayonunuliwa" na mwanamme. Kama ndoa ni upendo, na inatakiwa kuwa ya usawa, kwa nini mahari itoke kwa mwanamme kwenda kwa mwanamke? Kwa nini kuwe na mahari? Naweza kuelewa a mutual exchange of symbolic gifts, lakini hizi exhorbitant mahari zinakuja kufanya mwanamme aonekane kama anamnunua mke. Mwisho dada wa mume wanasema "tumekutolea ng'ombe arubaini, tufulie nguo zetu".
Kinachotakiwa sio tu kukemea wanaume wanaoendekeza udhalilishwaji wa wake zao, bali mfumo mzima unaomnyima mwanamke nguvu za kiuchumi na kumfanya awe chombo cha mwanamme na familia yake. Si haki kumkemea mwanamme tu wakati yeye ana dada zake ambao nao wanaendeleza ukandamizwaji wa mwanamke mwenzao. Vita dhidi ya ukandamizwaji wa wanawake isigeuke vita ya jinsia kati ya wanaume na wanawake. Kuna wanaume na wanawake wanaokandamiza wanawake kama vile kulivyo na wanaume na wanawake wanaotetea haki za wanawake.
Nilipofikiria nikaona kwamba kuna ukweli mwingi ndani yake. Embu fikiria ukiwa na mawifi wasiojua kutulia kwao, na kwako wakija ni maneno tu alafu kaka yao nae akawa anawaacha tu na kupuuza malalamiko ya mke wake nini kitatokea?
Mawifi wataendelea au hata kuzidisha mbwembwe zao pale, mke atakasirika kwa kuingiliwa na mawifi + kupuuzwa na mume hivyo kupunguza au hata kuondoa maelewano kati ya mume na mke.
Wanaume nyie ndio wenye jukumu la kuhakikisha familia zenu (mama, baba,dada na kaka) wanaelewa kwamba nafasi yao ni tofauti na ya mke wako.
Hili ni jukumu la wote. Naelewa kwamba ni rahisi kwa mwanamme kuwasiliana na familia yake zaidi ya mke wake, hasa kama kuna tension. Lakini mwanamke naye anatakiwa kuwa na msimamo. Wanaume wengi wangeweza kupewa motisha zaidi kuwakemea dada zao kama wanawake wengi wangekuwa na ujasiri zaidi wa kutoa msimamo. Lakini tunarudi bado kwenye swala la mfumo wa uchumi uliojengwa katika mfumodume. Hat kama kuna exception chache siku hizi ambazo baba na mama wanafanya kazi, traditionally baba ndiye breadwinner wa familia, na kwa hilo wanawake wengi huona kum confront baba squarely kunaweza kuharibu dynamics za kiuchumi ndani ya nyumba. Mke anaogopa kuambiwa "Unataka kunigombanisha na ndugu zangu" anaumia kimya au kwa kusema chinichini. This is not blaming the victim, it is a mere wake up call.
Kwamba ukishaoa unakua na familia nyingine ambayo kwa kiasi kikubwa inatakiwa ijitegemee (uongozi na maamuzi ndani ya nyumba) hivyo hawaruhusiwi kuingilia iwapo hamjawaomba kufanya hivyo.
Ukweli ni kwamba hii (nuclear family) ni concept ya kimagharibi zaidi na kwetu kama nilivyosema hapo juu, mwanamke "anaolewa" na mume na pengine na familia ya mume. Kutegemea na mazingira na mambo kama kisomo, uwezo wa kiuchumi, tamaduni na exposure. Lakini wabongo wengi hawana utamaduni wa nuclear family. Mimi nishaona mshkaji wangu (mbongo) kaharibu katika ndoa yake, mkewe (mmarekani) akawa anajaribu kumsemea kwa kaka yake, kaka mtu kamwambia dada yake "matatizo yenu ya ndani ya nyumba muyamalize wenyewe ndani ya nyumba". Nikaona hawa watu wako tofauti, angekuwa mbongo lingekuwa zogo hapo. As it turns out uamuzi ule ulikuwa wa busara kiasi kwani wanandoa walipatana na shemeji akaendelea kuwa na mahusiano nao mazuri wote. Imagine angeingilia kwa kumtetea dada yake, halafu wanandoa wapatane, jamaa angemuona mduanzi siku zote.
Na inapotokea wakajaribu uwaeleze kwamba hivyo sivyo mambo yanavyoenda. Badala ya kumwambia mkeo awavumilie tu, wakalishe ndugu zako chini uwaeleze kwamba mkeo hayuko pale kwaajili yao, kama wanaona anayofanya hayawapendezi wao ilhali wewe huna tatizo nayo basi nao watafute maboma yao ili wakafanye mambo wapendavyo huko. Usiruhusu maneno maneno ya ndugu zako yamkoseshe mkeo raha, hata kama ni madogo. Ndugu zako ndio wanaotakiwa kuBEHAVE na sio mke wako KUWAVUMILIA.
Kuna tabia nyingine ziko deep rooted na zimetiliwa mbolea ya miaka mingi ya malezi. Wewe familia ina watoto saba, mumeo kitindamimba na mwanamme pekee, matokeo yake kaishia kuwa mtoto wa mama na kazoea kuwa protected na dada zake (sisemi kwamba watu wa hivyo ndizo tabia zao, mfano tu). Anakuoa, hujafanya uchunguzi wa kutosha kumjua yeye na historia yake katika familia. Baada ya kuolewa unakuta vituko vya mawifi. Unajaribu kumbadilisha mtu. Good luck.
Hapa ndipo inapokuja sehemu ya kuchunguzana kabla ya kuoana. Zamani kabla ya kuona watu walikuwa wanafanya uchunguzi wa kutosha. Siku hizi watu wanakutana Facebook, washapanga mipango ya kuoana hata kabla hawajaonana, wakionana wiki mbili wametangaza ndoa, ndoa fasta kuliko quickies za Las Vegas. Matokeo yake umeoa ndoto kama wanavyosema "man of my dreams" lakini hawajamuoa mtu halisi.
Kwa hiyo kuepuka "majuto mjukuu" mchunguze mtu wako, ikibidi hamna kuoana bila ya uchumba wa kuwa karibu kwa kipindi cha angalau miezi sita.
Heri ya mwaka mpya. . . . natumaini utakua mzuri kwetu sote.
Na wewe pia.