Nafasi za chuo na mkopo kwa form for

Nafasi za chuo na mkopo kwa form for

mapengo junior

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2011
Posts
1,135
Reaction score
276
HABARI kama unae ndugu alie maliza form4 kuanzia 2009-2013 alie soma masomo ya sayansi (direct entery) ambae alipata Division 1,2 au 3 na angalau "C" moja kwenye masomo ya combination na "D" katika masomo mengine matatu kati ya Bios, Kemia, Fizikia, Elimu ya Lishe, Kilimo na Ufundi.

2.mwombaj mwenye sifa mbadala(equivalent) awe na ufaulu usiopungua kiwango cha D katika masomo ma3 kati ya Bios, Kemia, Fizikia, Elimu ya lishe, Kilimo na Ufundi, awe na astashahada (certificate) katika program za sayansi.

Mwambie aombe UDOM kwa mwaka wa masomo 2014/2015 utakao anza oktoba2014 kwa ajili ya kusoma Diploma ya ualimu wa sekondari na atapata mkopo wa ada, malazi, chakula, vitabu na viandikwa kutoka loan board(HESLB). Kwa maelezo zaid tembelea UDOM-WEB.

Ili kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati katika shule za Sekondari nchini,Wizaraya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) imeandaa mafunzo ya stashahada maalumu ya Ualimu katika Sayansi, Teknohama na Hisabati kwa wahitimu wa kidato cha nne na wale wenye sifa mbadala.

Mafunzo yatatolewa katika Chuo cha Elimu, Chuo Kikuu cha Dodoma. Mafunzo haya yatakayofuata mfumo wa Tuzo za Elimu ya Ufundi (NTA) unaoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) utamuwezesha mhitimu wa kidato cha nne kupata mafunzo maalumu.

Ili kufanikisha mafunzo haya maalumu, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu itatoa mikopo kwa wanafunzi wote watakaochaguliwa. Pamoja na serikali (wizara) kutoa nafasi ya mikopo kwa watakaofanikiwa kujiunga, programu hii ya mafunzo itawezesha wahitimu kupata ajira baada ya kuhitimu katika ngazi ya stashahada (NTA Level 6).

Baada ya kufanya kazi kwa muda usiopungua miaka miwili kama mwalimu mwenye Stashahada, mhitimu atakuwa na hiari ya kurudi chuoni kwa mafunzo zaidi ya Shahada ya Ualimu wa Sayansi, Teknohama na Hisabati (NTA Level 8). Mhitimu wa stashahada anayo hiari pia kupata mafunzo ya mwaka mmoja na kupata stashahada ya juu ya ualimu (NTA Level 7).

Mwombaji awe ni Mtanzania mwenye sifa
zilizoainishwa katika moja ya makundi kama
ifuatavyo:

(i) Kundi la I: Mwombaji wa Moja kwa Moja
(Direct Entry)
  • Awe amehitimu Kidato cha Nne ndani au nje ya nchi kuanzia mwaka 2009 hadi 2013;
  • Awe na ufaulu wa Daraja la I, II au III;
  • Awe na ufaulu usiopungua kiwango cha C katika moja ya somo la Tahasusi (combination) na D katika masomo mengine matatu kati ya Biologia, Kemia, Fizikia, Elimu ya Lishe, Kilimo na Ufundi.

(ii) Kundi la II: Mwombaji Mwenye Sifa Mbadala au sifa za Nyongeza (Equivalent/Alternative Qualifications)
  • Awe na ufaulu usiopungua kiwango cha D katika Hisabati na masomo mengine matatu kati ya Biologia, Kemia, Fizikia, Elimu ya Lishe Kilimo na Ufundi;
  • Awe na astashahada ya msingi (Basic Technician Certificate – NTA level 4) au Astashahada (Technicians Cerificate NTA level 5) katika programu za Sayansi au Sayansi shirikishi (Science or Allied Science) kama zilivyoambataishwa kwenye jeduali hapo chini; na
  • Awe na ufaulu wa wastani wa daraja B au GPA ya 2.7 katika mafunzo ya astashahada ya msingi au astashahada;
 
HABARI kama unae ndugu alie maliza form4 kuanzia 2009-2013 alie soma masomo ya sayans(direct entery) ambae alipata Division 1,2 au 3 na angalau "C" moja kwenye masom ya combination na "D" ktk masom mengine matatu kati ya Bios,Kemia,Fizikia,Elimu ya Lishe,Kilimo na Ufundi.
2.mwombaj mweny sifa mbadala(equivalent) awe na ufaulu usiopungua kiwango cha D ktk masom ma3 kati ya Bios,Kemia,Fizikia,Elimu ya lishe,Kilimo na Ufundi, awe na astashahada (certificate) ktk program za sayansi. Mwambie aombe UDOM kwa mwaka wa masomo 2014/2015 utakao anza oktoba2014 kwa ajili ya kusoma Diploma ya ualimu wa sekondari na atapata mkopo wa ada,malazi,chakula,vitabu na viandikwa kutoka loan board(HESLB). Kwa maelezo zaid tembelea UDOM-WEB.

deadline ya kutuma maombi ni lini?
 
HABARI kama unae ndugu alie maliza form4 kuanzia 2009-2013 alie soma masomo ya sayans(direct entery) ambae alipata Division 1,2 au 3 na angalau "C" moja kwenye masom ya combination na "D" ktk masom mengine matatu kati ya Bios,Kemia,Fizikia,Elimu ya Lishe,Kilimo na Ufundi.
2.mwombaj mweny sifa mbadala(equivalent) awe na ufaulu usiopungua kiwango cha D ktk masom ma3 kati ya Bios,Kemia,Fizikia,Elimu ya lishe,Kilimo na Ufundi, awe na astashahada (certificate) ktk program za sayansi. Mwambie aombe UDOM kwa mwaka wa masomo 2014/2015 utakao anza oktoba2014 kwa ajili ya kusoma Diploma ya ualimu wa sekondari na atapata mkopo wa ada,malazi,chakula,vitabu na viandikwa kutoka loan board(HESLB). Kwa maelezo zaid tembelea UDOM-WEB.

jinsi ya kutuma maombi ni kwa njia ipi?
 
Back
Top Bottom