Nafasi za kazi AKO Group Ltd

Nafasi za kazi AKO Group Ltd

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
4,876
Reaction score
1,549
AKO Group Ltd inayofanya kazi zake Barrick Gold Mine (Bulyanhulu) inakaribisha maombi ya watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 5 za kazi katika idara ya Usafi (Housekeepers) kutoka katika vijiji/maeneo yanayouzunguka mgodi

MAJUKUMU MUHIMU USAFI(HOUSEKEEPER)

  • Kusafisha vyumba vya wateja na mazingira yake kwa kiwango kinachohitajika na kampuni
  • Utunzaji wa vifaa vyote vya usafi na vya wateja kwa ujumla
  • Utekelezaji wa kiwango cha juu cha huduma kwa wateja ukiwa mgodini
  • Kuhudhuria vikao vya utendaji kazi kila siku na muda uliopangwa
  • Kutunza siri za kampuni
  • Kufuata utaratibu na maelekezo mengine yote atakayopangiwa na kiongozi wake

VIGEZO
  • Elimu kidato cha nne na kuendela
  • Cheti katika fani ya Hotelia
UZOEFU UNAOHITAJIKA
  • Uzoefu usiopungua mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na kufahamu mambo yote mhimu katika fani husika
  • Uzoefu wa kupokea malalamiko na kuyatatua kwa wakati
  • Awe anafahamu kusoma na kuandika (kiingereza ni muhimu zaidi)
  • Awe na uzoefu wa kufanya kzi katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano atapewa kipaumbele

Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au iingereza pamoja na wasifu CVs yapelekwe katika ofisi za AKO mapokezi au tuma kwa barua pepe eemmanuel@akogrouo.co.tz

Kama haujapigiwa simu na AKO ndani ya siku 5 baada ya siku ya mwisho ya kupokea maombi, basi ujue ombi lako halijafanikiwa utajaribu tena wakati mwingine

Tuma maombi kablaya tarehe 14/05/2020 saa 11:00 jioni
 
Ni siri gani hizo hadi housekeeper azitunze. Kama hadi mahauosekeeper watazijua siri za kampuni basi hizo siyo siri ni hoja za kampuni.

Kila la kheri kwa waombaji.
 
Back
Top Bottom