Jamii Opportunities
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 4,876
- 1,549
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na Wakala wa Vipimo anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi 4 kama zilivyo ainishwa katika tangazo hili.
MVUVI MSAIDIZI DARAJA LA II (FISHERIES ASSISTANT II) – NAFASI 1
MAJUKUMU YA KAZI
SIFA ZA MWOMBAJI
Wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye stashahada (Diploma) aidha ya Uvuvi au Uhifadhi wa Samaki na Masoko (Fish Processing & Marketing) kutoka vyuo vya uvuvi vya Mbegani, Kunduchi au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C
WAKALA WA VIPIMO
Wakala wa Vipimo ni Taasisi (Wakala) ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Wakala huu uliundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245, mapitio ya mwaka 2002.
Wakala wa Vipimo ilianzishwa rasmi tarehe 13 Mei, 2002 kwa amri ya Serikali Na. 194 (Government Order No. 194) na kutangazwa tarehe 17 Mei, 2002. Wakala wa Vipimo ina jukumu la kumlinda mlaji kwa kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika katika sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.
AFISA VIPIMO DARAJA LA II- NAFASI 3
MAJUKUMU YA KAZI
SIFA ZA MWOMBAJI
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mshahara ya Wakala wa Serikali yaani WMAS 3 kwa mwezi.
MASHARITI YA JUMLA KWA WAOMBAJI.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; Tanzania(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
Muhimu: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa
Katibu,
Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Bararaba ya 8, Kivukoni
S.L.P 63100 Dar es Salaam.
MVUVI MSAIDIZI DARAJA LA II (FISHERIES ASSISTANT II) – NAFASI 1
MAJUKUMU YA KAZI
- Kutengeneza, Kushona, Kutunza na Kukarabati zana za uvuvi;
- Kutunza na kuangalia mabwawa ya samaki;
- Kutega mitego Ziwani au Baharini;
- Kutengeneza nyavu ndogo ndogo;
- Kuwapa chakula samaki katika mabwawa;
- Kuvua samaki katika mabwawa;
- Kutoa ushauri kwa wavuvi kuhusu mbinu mbalimbali za uvuvi;
- Kukusanya takwimu za uvuvi kutoka kwenye vituo vya kupokelea samaki;
- Kutoa ushauri juu ya uhifadhi wa samaki na mbinu za usambazaji na uuzaji wa mazao yatokanayo na samaki;na
- Kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa samaki na mambo muhimu ya kuzingatia.
SIFA ZA MWOMBAJI
Wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye stashahada (Diploma) aidha ya Uvuvi au Uhifadhi wa Samaki na Masoko (Fish Processing & Marketing) kutoka vyuo vya uvuvi vya Mbegani, Kunduchi au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C
WAKALA WA VIPIMO
Wakala wa Vipimo ni Taasisi (Wakala) ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Wakala huu uliundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245, mapitio ya mwaka 2002.
Wakala wa Vipimo ilianzishwa rasmi tarehe 13 Mei, 2002 kwa amri ya Serikali Na. 194 (Government Order No. 194) na kutangazwa tarehe 17 Mei, 2002. Wakala wa Vipimo ina jukumu la kumlinda mlaji kwa kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika katika sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.
AFISA VIPIMO DARAJA LA II- NAFASI 3
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua, kuhakiki na kuvirekebisha vipimo vya wafanyabiashara;
- Kutunza na kuhifadhi vifaa vya kitaalamu vitumikavyo katika utendaji wa kazi;
- Kutoa ushauri kuhusu masuala ya uhakiki na matumizi ya vipimo;
- Kufanya upelelezi kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya vipimo; na
- Kupokea na kufanyia kazi malalamiko ya wadau na wateja;
SIFA ZA MWOMBAJI
- Shahada ya kwanza katika fani ya Legal Metrology au Legal and Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;
- Shahada katika fani ya Uhandisi au Sanyansi ambao wamepata “crash programme in Legal and Industrial Metrology” isiyopungua miezi minne (4) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;
- Shahada katika fani ya Uhandisi au Sayansi ambao wamehitimu Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika fani ya Vipimo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;
- Stashahada ya juu katika fani ya Legal Metrology au Legal and Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mshahara ya Wakala wa Serikali yaani WMAS 3 kwa mwezi.
MASHARITI YA JUMLA KWA WAOMBAJI.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa;
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo;
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika;
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA;
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE);
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi;
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010;
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria;
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 26 Novemba, 2019.
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.