Nafasi za kazi zinazotangazwa JF.

Jaluo_Nyeupe

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
2,824
Reaction score
2,264
Wakuu nimekuwa nikiwatafutia kazi jamaa zangu kupitia nafasi za kazi zinazotangazwa humu JF. Lakini mara nyingi nimeshindwa kuelewa baadhi ya kazi zinazotangazwa humu hasa kutoka Zoom Tanzania kama ni utapeli ama lah. Mfano kuna nafasi za kazi kutoka Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) za tar 26 jan ambazo zoom tanzania wametangaza bila kuonyesha source ya tangazo lao kama ni gazeti fulani au ni kampuni yenyewe imewatumia tangazo hilo www.jamiiforums.com/nafasi-za-kazi-na-tenda/216310-nafasi-za-kazi-34-tarehe-26-januari.html. Sasa ukienda kwenye Web site ya TIRA www.tira.go.tz/work/index.php unashangaa hakuna nafasi za kazi. Hapo nashindwa kuelewa kwamba ni baadhi ya makampuni wanachelewa ku-update website zao au ni utapeli unaofanywa na hawa wanaotuletea matangazo humu?
 
Zoom Tanzania wao wanatangaza nafasi kama zinavyofikishwa na wahusika wenyewe. Zoom pia ni source hivyo hauna haja ya kutaka kuwa na source zile ambazo unaziamini wewe binafsi. Mfano mimi binafsi nimeitwa ktk interview nyingi kupitia application zilitoka hapo zoom pekee na wala kulikuwa hamna link wala source ya Magazeti.
 

Naona hatujaelewana, sijasema matangazo ya zoom sio ya kweli au siamini source yao. Mimi mwenyewe nimefaidika na baadhi ya matangazo yao. Tatizo ni pale unapoona tangazo la kazi limetangazwa hapa JF halafu unapofuatilia unagundua halipo. Nimetoa hizo link kama mfano unaweza kuzifungua na kuelewa ni nini ninachomaanisha hapa..
 
Mkuu tatizo linakuwaga kwa websites za hizo kampuni zinazotoa nafasi za kazi.
Huwa hawa update websites zao, so unapozitembelea baada ya kuona nafasi za kazi let say umeziona zoom, unakosa taarifa kwa kuwa wao wenyewe kwenye webites zao hakuna information mpya.
 
hzo nafasi kweli zmetangazwa hata kwny gazeti la Daily news la tarh 25 zipo.
 


Jibu la maswali/swali lako liko kwenye hiyo red.
 
Mkubwa. Sio makampuni au mashirika yote yenye utaratibu wa kutangaza nafasi za kazi kwenye websites zao, hivo unaweza kupewa link labda kukufahamisha ofisi iliyotoa tangazo hilo la kazi. mie nimeona matangazomengi zoom yakiwa na link lakini ukiifuatilia hiyo link hulikuti hilo tangazo huko, ila kinachotokea unaapply na baadae unasikia kuna interview zimefanyika.
Mie nafikiri hilo lisikusumbue.
Best wishes bro
 
Nashukuru kwa majibu yote ambayo yamekwishatolewa.

Kazi zote unazoziona kwenye ZoomTanzania.com, zinatokana na vyanzo vikuu viwili:
  • Mhusika wa kampuni husika ana-post kwenye Website Yetu
  • Mhusika wa ZoomTanzania.com ana-angalia nafasi za kazi zilizo kwenye magazeti, na kuzi-post.
Ili kutofautisha vyanzo hivi tofauti, nafasi zote ambazo mhusika wa ZoomTanzania anazipost, zinakuwa na taarifa kuwa zimetoka kwenye gazeti fulani. Magazeti tunayotumia ni Daily News na The Guardian. Ukiangalia magazeti hayo ni lazima utazikuta kazi hizo tulizopost. Inawezekana pia, zikawemo katika magazeti mengine.

Ni kweli pia kuwa baadhi ya makampuni website zao ni 'static', yani hazibadiliki mara kwa mara. Hivyo wengi huwa hawatangazi nafasi zao kupitia website zao.

Tunaendelea kuwasisitiza wana JF kuwa, ingawa tunachuja nafasi zote za kazi zinazokuja kwenye Website yetu, bado tunachangamoto kubwa ya mbinu mbalimbali wanazotumia matapeli, ukiona kazi yoyote yenye utata, tafadhali tujulishe na tufuatilie zaidi.

Tunashukuru sana kwa changamoto na mawazo mnayotupa.

Nawatakia siku njema,

Pendo Gerald,
ZoomTanzania.com
 

tuwajulishe kupitia nn?
 

Wewe ndie unajichanganya, anayepost hapa Jamii forums kwa niaba ya Zoom Tz ni Toto lucky na application details huwa anaziweka ktk link ya Zoom Tz ndio maana nikajibu hivyo. Inachotakiwa Kujua Kuwa hapa Jf au Zoom Tz watu ndio wana upload hizo kazi hivyo sisi waombaji ndio tupambanue zaidi.
 
hi, me namuunga mkono totolucky, ni kweli nafas za kaz wanazotangaza zoom pia wanazicopy kwenye magazeti kwa mfano tangazo la nafasi za kazi Arusha technical college niliziona juzi kwenye gazeti kama sikosei ni gazeti la mwananchi au nipashe ya ijumaa january 27, 2012. soo zoom ni mambo yote nawapongeza sana zoom mpo juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…