Jaluo_Nyeupe
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 2,824
- 2,264
Wakuu nimekuwa nikiwatafutia kazi jamaa zangu kupitia nafasi za kazi zinazotangazwa humu JF. Lakini mara nyingi nimeshindwa kuelewa baadhi ya kazi zinazotangazwa humu hasa kutoka Zoom Tanzania kama ni utapeli ama lah. Mfano kuna nafasi za kazi kutoka Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) za tar 26 jan ambazo zoom tanzania wametangaza bila kuonyesha source ya tangazo lao kama ni gazeti fulani au ni kampuni yenyewe imewatumia tangazo hilo www.jamiiforums.com/nafasi-za-kazi-na-tenda/216310-nafasi-za-kazi-34-tarehe-26-januari.html. Sasa ukienda kwenye Web site ya TIRA www.tira.go.tz/work/index.php unashangaa hakuna nafasi za kazi. Hapo nashindwa kuelewa kwamba ni baadhi ya makampuni wanachelewa ku-update website zao au ni utapeli unaofanywa na hawa wanaotuletea matangazo humu?