Nafikilia kutengeneza ndege!!

Nafikilia kutengeneza ndege!!

edgar90

Senior Member
Joined
Jun 18, 2016
Posts
145
Reaction score
116
Bilashaka mnaendelea vizuri wanajamii forumn !! Niende kwenye mada!! Binafsi hua Nina ndoto ya kutengeneza ndege lakini hua sijaifanyia kazi,sasa baada ya yule kijana wa tunduma kutengeneza helikopta ni kama amenichochea ile ndoto yangu kwa sababu tangia nipo form six nilikua nikijifunza masuala ya ndege,sehemu zake na jinsi zinavyofanya kazi!!

Sasa naomba msaada wenu mimi nimtaalamu wa masomo ya physics na mathematics na nimejaribu kufanya research how to build ultralight aircraft at home ,nimetumia mda mwingi sana ili nitakapoanza kutengeneza basi nihakikishe ndege ina take off Sio kama wa tunduma japo alijaribu!

Mimi ni mtumishi wa serikali!!
 
Huwezi kuamka asubuhi ukasema natakakutengeneza ndege kuna procedures Za ku follow up
 
Bilashaka mnaendelea vizuri wanajamii forumn !! Niende kwenye mada!! Binafsi hua Nina ndoto ya kutengeneza ndege lakini hua sijaifanyia kazi,sasa baada ya yule kijana wa tunduma kutengeneza helikopta ni kama amenichochea ile ndoto yangu kwa sababu tangia nipo form six nilikua nikijifunza masuala ya ndege,sehemu zake na jinsi zinavyofanya kazi!!

Sasa naomba msaada wenu mimi nimtaalamu wa masomo ya physics na mathematics na nimejaribu kufanya research how to build ultralight aircraft at home ,nimetumia mda mwingi sana ili nitakapoanza kutengeneza basi nihakikishe ndege ina take off Sio kama wa tunduma japo alijaribu!

Mimi ni mtumishi wa serikali!!

Ndugu wazo lako ni zuri na itakuwa vema sana ukilifanyia kazi na ukafanikisha.
Naomba tuwasiliane Private Message.
 
Ukijitahidi saaaana labda kuasemble tu. Huo ni ufundi wa kawaida, lakini kutengeneza sisi teknolojia hiyo hatuan. Hata huyo jamaa wa tunduma aliasemble tu, hakuna alichotengeneza pale
 
My slogan state that "the power of idea is from action"
already you have idea now take action to make your idea to exist
 
Una ndoto kama nilizokuaga nazo mimi, ila nilishafika point ya kukubali kwa hali ya maisha ya tanzania ni ngumu sana kufikia hilo lengo... ila tunachoweza fanya ni kuunganisha nguvu tutengeneze flight simulators, ambazo tunaweza zitumia kuanzisha mafunzo ya watu wanaotaka jifunza urubani, japo hata hilo nalo lina changamoto sana.. ila kwangu ndio ndoto yangu, hii ina usalama zaidi... Nina miaka 28, nimeoa na nina Masters Degree ya Intenational Business lakini mapenzi yangu siku zote yamekua maswala ya anga
 
nategemea iona hiyo yako kwenye uzinduzi wa mwenge mwakani
 
Nyoo. Kiswahili tu shida ndo ndege utaweza?
Eti nafikilia badala ya nafikiria !
 
Kila la kheri, ila kutengeneza ndege sio kazi ndogo, mi ningeshauri kwanza utengeneze hata drone ili upate demo ya Bernoulli principle na newton laws jinsi zinavyoweza Ku apply maana hapo itabidi upate injini ambazo zina HP zinazozarisha RPM kubwa kiufupi ni gharama Sana, ila Kama unataka vitabu ili zaidi utafiti mi ninavyo.
 
Jamani mie nimeanza kutengeneza bunduki, nilianza tangu mwaka 2009 kwa kuandaa mchoro but now nimeanza kuunga pole pole but nahisi itakua na mlio mkubwa sana maana nimekosa utaalamu wa kupoza mlio, tayari nimeanza kushughulikia Kibali na nimeshafikia hatua nzuri na mchoro nilipeleka kunakohusika. Nategemea miaka 3-5 ntakua nimekamilisha wakuu. Ni bunduki nzuri sana na itakua na uzito wa around 5.8kgs ukiwa full magazine (risasi 19x2=38)
 
Soon utafungwa wewe!!
 
Kwenye hali kama hii tutasema nini sasa?...Maisha hayaeleweki,tunawaza kutengeneza ndege na tunataka kufanya mambo makubwa zaidi lakini mazingira si rafiki.Anyway dreams are valid,keep dreaming.
 
Back
Top Bottom