Nafikiri Mwamposa (Bulldoza) ana Kesi ya Mauaji

Nafikiri Mwamposa (Bulldoza) ana Kesi ya Mauaji

uttoh2002

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
17,060
Reaction score
32,400
Kwa heshima na moyo wa masikitiko nawaombea faraja wafiwa wote katika Ibada ya Mwamposa!

Ninaimani serikali yangu sikivu haitalifumbia hili macho ili kuweka standard katika namna ya ku deal na hawa manabii fake!

Mtu anapoitisha kongamano na kupata kibali anawajibika kuangalia usalama wa watu wanaohudhuria na kuhakikisha wapo salama.

Nina maswali tu Machache ya kuuliza:

1. Kwa nini hapakuwa na utaratibu wa kuratibiwa wa kufuata huo upako wa kueleweka?

2. Hapakuwa na ushers ambao wanakuwa katikati wakisimamia mambo yote yanayoendelea?

3. Je mazingira ya eneo mlilofanyikia kongamano palikuwa ni salama kwa kuangalia idadi na kuja kitu?

4. Kuna Watoto wanne pia wamekufa, ni namna gani waliiweka ya kuweka uwiyano wa Watoto nawatu wazima?

Nafikiri ni wakati Serikali yetu iangalie haya mambo ya manabii kwa Kina, na iwasadie wananchi wake!
 
Kipengere kipi cha sheria kinampa bulldoza kesi ya kujibu?
 
Kibali cha Mkutano mwisho ilikuwa saa 11 jioni yeye akaendelea hadi saa 2 usiku
bora angejiua km Kibwetere wa Uganda
kuweka beseni moja hata halina eneo la skwea mita moja halafu mlango mmoja
hawa watu sasa wapigwe marufuku mpaka wawe na Digrii sio Makonda kuwatetea kila siku ni Maombi na kazi hawafanyi utafikiri wamekuwa ndege
waanze kulipishwa kodi, kwa mikusanyiko hiyo
kuwapoteza watu 20 halafu unakimbia ni dharau
 
Back
Top Bottom