Nafikiri Nokia wajitafakari kwenye suala la smartphone na viswaswadu

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
4,031
Reaction score
6,156
Kama Nokia anataka kurudi ajitafakari Sana bado ana nafasi.

Simu za Nokia ZOTE smart na viswaswadu ni GHALI kishenzi LAKINI Zina hardware mbovu Sana hasa KWA smart za SASA .

Naposema hardware mbovu sina maana hazidumu ninamaanisha hardware zisizo na performance nzuri, mfano camera, zinaganda Sana na kichemka au wakati mwingine kuzima na kuwaka hii NI KWA smart.


KWA viswaswadu hapa wamejitahidi Shida KUBWA ni feature ndogo Bei KUBWA Sana.


Kama watajitahidi kuleta vitu vizuri wahakikishe ni affordable.

Siwezi nunua kiswaswadu KWA laki 2 au 120k viswaswadu VYOTE vinatakiwa KUWA chini ya 40k labda kama vina feature za android BASI 70k
 
Hao wameshindwa ila hawataki kukubali ,nilitumia sana hizo simu zao ; nokia Asha na Express music.

Kwa sasa hawana jipya haga kuwafikiri ni zaidi ya miaka 10 ..
 
Tafuta hela, acha kushauri watu ambao hata ushauri wako hawauoni wala kuutambua au unadhani mkurugenzi wa Nokia anaishi Buza kwa Mparange?
 
NOKIA hawatengenezi tena simu
Hizo smartphone za Android unazoona zinaitwa Nokia zinatengenezwa na kampuni ya HMD Global, nayo ni ya hukohuko Finland
Na sasahivi HMD wameacha kutengeneza simu kwa jina la Nokia, wameanza kuziita HMD
Hii kampuni simu zake (kuanzia Nokia hadi HMD) sio value for money, ni overpriced na performance ni ya kawaida sana. Kama mtu anataka midrange ni heri anunue Redmi au Samsung A series
Hata Tecno na Infinix simu zao ni nzuri kuliko hao HMD
 
"Hatujafanya kosa lolote ila kwa mamna flani tumepoteza"
NOkia CEO
 
Wakuwalaumu ni HMD. Nokia yeye anakula hela yake kwa jina maana Kwenye biashara ya simu alishaachana nayo.
Anakulaje checki HIZI Nokia ninefululiza natumia Nokia 1 MPAKA 5
 
Hapa uneeleweka vipi ZILE Nokia 1, Nokia 2, 3 ...
 
Nokia kaacha kutengeneza simu toka 2013, na wanaotumia jina la Nokia kutengeneza simu hawauzi ghali hivyo. Juzi nimenunua hicho kiswaswandu 20,000 na bado hapo nimemuachia mtu faida.
Acha viswaswadu vya Nokia 110 jitafutie Nokia 215, 5310 latest hapo kkoo unipe Bei yake nanunua oppo used f series
 
Anakulaje checki HIZI Nokia ninefululiza natumia Nokia 1 MPAKA 5
We Google simu yako ukiona imetengenezwa baada ya 2013 jua haijatengenezwa na Nokia.

HMD, flipkart, TCL, Off global, RICHGO, streamview etc wote wanatumia brand za Nokia, wanatengeneza wao vifaa na kununua jina la Nokia na kuweka.

Kifaa pekee cha Nokia utakachopata mtaani ni zile Router wanazotumia Vodacom, Nokia Beacon.

Na kutofautisha Nokia OG zina logo yake na Nokia ambazo zimekua licenced zina logo yake.

Logo mpya wanayotumia Nokia sasa hivi.


Picha ya WiFi router ikiwa na Logo mpya.
 
We Google simu yako ukiona imetengenezwa baada ya 2013 jua haijatengenezwa na Nokia.

HMD, flipkart, TCL, Off global, RICHGO, streamview etc wote wanatumia brand za Nokia, wanatengeneza wao vifaa na kununua jina la Nokia na kuweka.
So HATA viswaswadu sio nokia
 
Wakuwalaumu ni HMD. Nokia yeye anakula hela yake kwa jina maana Kwenye biashara ya simu alishaachana nayo.
Sasa hivi na wao wanatoa simu zao kwa brand hiyo ya HMD ila bado ziko chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…