Habari za muda huu hapa,
Naishi Dsm Nina familia ya mke na mtoto mmoja.
Kazi --nimeanza kufanya kazi ya ULINZI kwenye kampuni binafsi la Gardworld, nikiwa hapa hapa Dsm.
Maisha yamekuwa magumu sana na hakuna maendeleo yoyote nayoyaona zaidi ya kulipia Kodi,na kupata Hela ya kula basi,Ukizingatia huu ni mwaka wa 3 Sasa nipo kwenye kazi hii.
Awali tulikuwa tunalipwa 250k take home baadae ikaja kupanda Hadi 370k take home,kibaya zaidi LINDO nilililokuwepo mkataba ukafa ikabidi tupewe termination letter na watu wengi sana waliachishwa kazi ilikuwa 2022 kuingia 2023 ,nikasain garda west kama kampuni ndogo yake na mshahara kubakia 250k Tena.
Nimefanikiwa kununua eneo la eka Moja Morogoro.
Hii kazi Sasa naona niache nikafanye shughuli ata za kilimo shamba kuliko kuendelea kuteseka namna hii,unalala nje mbu wako, mvua yako,jua lako, mashanyanyaso mengi, hupati haki zako za Msingi.
Mawazo yenu wadau,au nitakuwa nakosea kuacha kazi hii ambayo haina manufaa zaidi sana ni kudumaza akili tu.
Elimu yangu nimesoma diploma ya Agri business lakini nimetuma maombi ya kazi mara nyingi sijabahatika kupata kazi ya career yangu.
Mshahara wa 250000 Kwa Jiji hili la Dsm naona napoteza muda wangu tu.
Naomba ushauri wowote nitasoma Kila comment.
Dahh pole sana.
Hii kazi niliwahi kufanya mwaka 2021 kampuni hyo hyo ya Garda world kwa muda wa miezi sita pale coca-cola.
Aisee hii kazi iskie tuu, lkn ni moja ya kazi sana yenye changamoto nyingi kama ifuatavyo.
1. AFYA NA UHAI.
Afya yako inakua hatarini kutokana na mkesha wa usiku kucha hivyo utapigwa na mbu, baridi Kali pamoja na viungo vya miwili kuchoka. Lakini pia maisha yako hatrn kutokana na vibaka wenye silaha.
2. MASLAHI HAFIFU.
Hapa mshahara utakaopata ni wakukusogeza NDANI ya mwezi husika lkn kuhusu malengo ni ngumu.
3. JELA.
Ukiwa mlinzi tegemea matatu yatakutokea endapo uvamizi wa majambazi utatokea. Kupambana nao wakupe kilema cha maisha ama wakuue au laa ukimbie lkn ujiandae na JELA.
MACHACHE MAZURI KUHUSU KAZI HII.
1. Unaweza kubahatika kupangiwa Malindo ya ubalozi Huwa wanalipa helanzuri .
2. Unaweza kupata promotion ya kuwa kiongoz lkn lazima uwe mnoko kwa wenzako.
3. Unaweza kupata LINDO ambalo halina changamoto sana hivyo kazi utaoyona nzuri.
HITIMISHO.
KWAKWEL wakati nafanya hii kazi nilijiambia moyoni , sikuja duniani kuwa mzinzi na hayo ndo yalikua majibu yangu hata kwa wale viongozi waliokua wanoko ambao ukisnzia tuu picha shwaaa.
USHAURI KWAKO NA VIJANA WENGINE WAPAMBANAJI.
Tafuta hata boda boda ya mkopo, komaa na Jiji MUNGU ATAKUSAIDIA ndugu yangu.
Kijana yeyote, katika maisha yako kazi iweke chaguo la mwisho kabisa baada ya kujaribu vitu vyote duniani hapa vimeshindikana.
Ile kazi ni kama mfungwa huru. Yani kila mtu wewe ni boss wako mpka mfagizi wa nyumba.
Nna mengi ila kwaleo yanatosha