Nafikiria kuanzisha Kiwanda cha Bati, Mashine zake bei gani?

Nafikiria kuanzisha Kiwanda cha Bati, Mashine zake bei gani?

Hiyo bei ya mashine ya kukunjia hizo bati mbona kama iko chini sana! Kuna uzi wa miaka kadhaa nyuma, kuna jamaa alikuwa anauza milioni 80!!
Machine mkuu bei zinaenda na specifications na uwezo wa kubend na kukata sheet utazoweka. Machine za kawaida zinaanzia usd 10,000 kuinunua.

Ukichagua zenye CNC Machine na computerised bei inakuwa kubwa sana hizi unaweka mchoro au aina ya mgongo unaotaka inakunja na kukata. Za kawaida unaset manual migongo inakata na kukunja kwa kuikomandi manual
 



Ongea na wachina. Pia ongea na watu wa silent ocean wanaweza kusafirishia mtambo. Na hata hizo rolls za kutengeneza bati wanasafirisha.
Uwe na eneo la kuzalishia la kukodi au kununua
Uwe na forklift ya kubeba rolls za kutengeneza bati toka kwenye roli hadi kwenye mtambo
Uwe na gari za kusafirishia bati (za kukodi, used za kibongo, au kununua)


Ujipange kwenye marketing ya mabati yako. Uwe na vijana wenye connection ya masoko ya mabati. Uwe na vijana wenye connection ya masoko ya mabati, bila ya kupata masoko ya mabati UTAPATA tabu Sana
 
Helloow mwenye taarifa za garama za kiwanda cha kushape bati anijuze,, nataka nianze kujipanga taratibu ndani ya miaka kazaa nianze uzalishaji asante

Kila la kheri mkuu.
 
1001346909.jpg
1001346909.jpg
Quotation ya Coil za kutengenezea bati zenye rangi. Hiyo bei ya kununua bila usafirishaji mpaka Tanzania
 
Back
Top Bottom