Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,319
Nasomea BA in Kiswahili, niko mwaka wa pili hapa Chuo Kikuu Dar es salaam. Karibuni nimejiwa na wazo la kubadili uelekeo wangu kikazi, nataka kuwa mwandishi wa habari, hasa habari za michezo nikijikita katika soka la Kiafrika.
Nia ninayo, sababu ninazo na uwezo ninao! Hii haimaanishi kuwa nitaacha kusome hiki nanachokisomea, la hasha! Nitamaliza kwanza kisha nikasome uandishi wa habari, au nianze kusoma diploma yake nikiwa namalizia bachelor.
Tangu utoto napenda soka, na kinachoniuma ni kuwa soka ya Kiafrika inapoteza mvuto dhidi ya soka la Ulaya, tena suala sio kiwango, bali ni kutokana na mkazo kidogo ambao inapata kutoka kwa wanahabari na vyombo husika.
Nimeshaandika makala moja ya ukurasa mmoja kwa wahariri wa The African na The Ciitizen, kama ikibahatika kuchapishwa nitawajuza.
Nakaribisha maoni, ushauri, mapendekezo, dislikes, majungu, hatings bila kusahau comments za 'napita tu'...
UPDATES; Almost there, jana nimehitimu basic certificate in Journalism hapa SJMC (zamani TSJ)