Nafikiria kubadilisha career..

Nafikiria kubadilisha career..

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Nasomea BA in Kiswahili, niko mwaka wa pili hapa Chuo Kikuu Dar es salaam. Karibuni nimejiwa na wazo la kubadili uelekeo wangu kikazi, nataka kuwa mwandishi wa habari, hasa habari za michezo nikijikita katika soka la Kiafrika.
Nia ninayo, sababu ninazo na uwezo ninao! Hii haimaanishi kuwa nitaacha kusome hiki nanachokisomea, la hasha! Nitamaliza kwanza kisha nikasome uandishi wa habari, au nianze kusoma diploma yake nikiwa namalizia bachelor.
Tangu utoto napenda soka, na kinachoniuma ni kuwa soka ya Kiafrika inapoteza mvuto dhidi ya soka la Ulaya, tena suala sio kiwango, bali ni kutokana na mkazo kidogo ambao inapata kutoka kwa wanahabari na vyombo husika.
Nimeshaandika makala moja ya ukurasa mmoja kwa wahariri wa The African na The Ciitizen, kama ikibahatika kuchapishwa nitawajuza.
Nakaribisha maoni, ushauri, mapendekezo, dislikes, majungu, hatings bila kusahau comments za 'napita tu'...
UPDATES; Almost there, jana nimehitimu basic certificate in Journalism hapa SJMC (zamani TSJ)
 
Bora ukimaliza ukasome masters in journalism and mass comm,nadhan inawezekana,pia kuandika michezo na makala za michezo sidhani kama unahitaji uwe umesoma journalism,hicho kiswahili pamoja na mapenz yako kwenye michezo inatosha katika uandishi,unahitaji pia kujiimarisha katika lugha nyingine hasa kingereza ili uweze kuandika kwa ufasaha
 
Wakati unachagua courses zako hukuiona hyo ya journalism jombaa? Kama vp komaa na ving'ong'o, kaptula la max etc then ukafanye postgraduate ya journalism and masscom!!
 
Wakati unachagua courses zako hukuiona hyo ya journalism jombaa? Kama vp komaa na ving'ong'o, kaptula la max etc then ukafanye postgraduate ya journalism and masscom!!

Soko la degree ya kiswahili ni kubwa ndani na nje kuliko hilo la uandishi wa habari.Soko la uandishi wa habari limefurika ndani na nje kupata ni kazi hasa by the time unamaliza utajikuta huna kazi utaanza kutukana serikali kuwa wasomi haiwapi ajira!
 
Hongera! Mafanikio huletwa na kufanya kitu unachokipenda. Kama potentials zako unadhani zipo huko, just do it. Wishing you all the best in your career.
 
Wakati unachagua courses zako hukuiona hyo ya journalism jombaa? Kama vp komaa na ving'ong'o, kaptula la max etc then ukafanye postgraduate ya journalism and masscom!!

Niliziona sana, na score nilikuwa nazo za kuniwezesha kujiunga, ila upenzi na lugha ulinizidi nikajikuta nachagua BAK.
Ushauri wako nitauzingatia.
 
Bora ukimaliza ukasome masters in journalism and mass comm,nadhan inawezekana,pia kuandika michezo na makala za michezo sidhani kama unahitaji uwe umesoma journalism,hicho kiswahili pamoja na mapenz yako kwenye michezo inatosha katika uandishi,unahitaji pia kujiimarisha katika lugha nyingine hasa kingereza ili uweze kuandika kwa ufasaha

nashukuru kwa ushauri mkuu...
Najua kuwa naweza kuandika makala bila kusomea uandishi, ila nadhani ningepata japo diploma ya Journalism ingekuwa vizuri zaidi.
 
Wazo zuri na hongera kwa kutaka kuendeleza kipaji chako. Kama walivyoshauri wadau ukasome postgraduate ya Mass and Com.

Ila kuwa makini na kauli zako kabla hujafanya tafiti. Waandishi hapa Afrika,tz wamejitahidi sana kutangaza habari la michezo lakini maendeleo ya michezo ulaya kuna factors nyingi sana ukiacha kutangazwa. Hapa Afrika hususan Tz mfumo wa michezo na sera kwa ujumla sio bombaaaa.....tumia lugha hii unataka kuwa mmojawapo wa kuendeleza michezo kwa njia ya kalamu/vinginevyo kuchangia pale walipoishia wengine au kwa kushirikiana nao.
 
Nteko Vano,
Nimekuelewa mkuu, nitajitahidi kuzingatia uliyonieleza. Kuhusu role ya wanahabari katika kudidimiza soka la Afrika sina shaka kabisa, angalau kipindi hiki sera za michezo zimejitahidi kupanua wigo kuliko hapo zamani, lakini bado mwamko wa watu kwa soka la ndani unazidi kudidimia. Leo mtoto wa miaka 8 anamfahamu vema Wayne Rooney lakini hawezi kuutambua uso wa Mbwana Samatta, unadhani hilo ni tatizo la sera?
 
Last edited by a moderator:
uamuzi ni wako. diploma in journalism = 1 to 2yrs, MA journalism = 1to 2 yrs.
 
unaweza kufanya hivyo lakini kama utabalance upepo wa kutafuta hela na matakwa ya roho yako hamna shida kabisa...
 
jitahidi kuanza kuandika makala za michezo na uanze kuzituma ktk magazeti/kwa mhariri then wqkiona ziko poa taratbu wataanzq kuzipublish then itakuwa ndio mwanzo huo... Huitaji kuwa proffessional at first sight.... Hakikish ni mweledi wa lugha nauandikacho kinamtirirko mzuri
 
uamuzi ni wako. diploma in journalism = 1 to 2yrs, MA journalism = 1to 2 yrs.

Thanks kaka, nimepata muda wa kufanya kozi fupi ya uandishi wa habari pale TSJ, nimeshaomba kujiunga kuanzia mwezi huu wa saba. Nadhani sio mbaya kwa kuanzia.
 
Komaa mtoto wa kiume

Nikikomaa mauzo yatapotea meen, si unajua si ndo wauza sura?
Jees kidding bro, thank you for such an inspirational short text, ki-kitaa zaidi.
 
Bora ukimaliza ukasome masters in journalism and mass comm,nadhan inawezekana,pia kuandika michezo na makala za michezo sidhani kama unahitaji uwe umesoma journalism,hicho kiswahili pamoja na mapenz yako kwenye michezo inatosha katika uandishi,unahitaji pia kujiimarisha katika lugha nyingine hasa kingereza ili uweze kuandika kwa ufasaha
umenena
 
Almost there mazee. Yesterday nimegraduate kwa skuli ya Uandishi joh, na vile nimepata certi.
 
Back
Top Bottom