Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 81
- 117
Habari wanaJF,
Ni mimi tena (It's me again). katika pita pita zangu, nimeangukia kozi moja makini ambayo naweza kuileta kwenu kwa ajili ya kusaidia wanaotaka kufanya kazi Upwork. Nina account huko, na nimefanikiwa pakubwa.
Kozi screenshot yake hii hapa:
Niliipata kwa mKenya fulani hivi rafiki yangu (na mwandishi pia), na inalenga kuwasaidia waandishi (na wenye profession zingine pia), kuelewa Upwork vizuri na kufine tune kwa ajili ya mafanikio yao.
Kozi ina sura 9, zifuatazo:
Baada ya kuona outline, naomba kuleta hoja zifuatazo ili tuende vizuri:
Natamani kupata watu walau 50 ambao wataonyesha nia (kwa vitendo tu). Nilitaka kufahamu kama hili ni hitaji, au watu wanasemaga tu "twenzetu tupate kazi mtandaoni". Kama ni hitaji, niko hapa kusapoti.
Niliamua kuwa sitoi misaada ya bure, hasa katika suala la maisha na biashara. Free things are always abused (vya bure hutukanwa/kudhalilishwa/kuchukuliwa poa). Ila, nilitaka nitoe huduma hii kwa bei rafiki za hapa nyumbani.
Swali: Huduma kama hii inaweza kuwa priced vipi ili kutunufaisha wote? Hili pia niliomba kulijua kutoka kwako/kwenu.
Swali: Nini kifanyike zaidi ya nilichokisema hapa? naleta hili pia.
Haya, mwisho wa nukuu. Twenzetu...

- How to Setup Your Upwork account like a Pro (Jinsi ya kuunda akaunti yako ya upwork kininja)
Hapa tutazungumzia Namna ya kuanza, Kutengeneza specialized profiles, kuunda eneo la portfolio, Kutumia project catalog, kutumia feature ya benchmarking.
(Homework: Mtaalam atakagua profile yako na kuona kama inafaa)
- How to select the right clients who will value you (Jinsi ya kuchagua wateja wanaoona thamani yako)
Hapa tutazungumzia namna ya kutafuta wateja wenye thamani (high value clients), na wateja wa kuwakimbia kama ukoma (clients from hell, clients to avoid).
- Proposal Writing Secrets that can Skyrocket your success (Siri za kuandika barua za kuomba kazi, zitakazokufanikisha)
Tutazungumzia jinsi ya kuandika proposal zinazolipa, kuelewa terminologies mbalimbali kama vile pricing (bei), milestones (hatua za kazi), screening questions (maswali ambayo waajiri hutumia kuchuja maombi ya kazi),
(Homework: Mifano ya barua zilizowahi kuleta ushindi, unazoweza kutumia kama inspiration na kutengenezea maombi yako ya leo na kesho)
- Negotiation Tactics to Help You Win Those Interviews (Namna ya kujitetea hadi kupata kazi)
Siri za kufanya waajiri watake kufanya kazi na wewe.
- Ways to Increase Your chances of getting 5-star reviews and Repeat jobs (Jinsi ya kuzidisha nafasi ya kupata alama za nyota 5 na kazi zinazodumu/kujirudia)
Utajua kile wanachotafuta wateja, na namna ya kuwapa wanachokitafuta mara kwa mara
- Useful Upwork features (Sifa njema za Upwork)
Jua sifa hizi muhimu zitakazokusaidia kuenjoy muda wako ukiwa Upwork
- How to Raise Your Rates (Jinsi ya kupandisha thamani ya fedha unazotoza upwork)
Hapa twende tararibu. Utapata mawaidha ya namna ya kuzidisha thamani ya huduma zako.
- Mistakes to Avoid (Makosa ya kuepukana nayo)
Hapa wengi inawahusu. Utajua vitu vya kuviepuka kabisa kama unataka mafanikio huko.
- Next Steps (Kinachofuata)
Ntakupa resources zaidi ya kujisomea na kujitafutia endapo utataka kufanikiwa.
Baada ya kuona outline, naomba kuleta hoja zifuatazo ili tuende vizuri:
- Hii Kozi ni kwa ajili ya wazoefu na wanafunzi wapya Upwork. Kuna sections za beginners, lakini pia kuna section ya wazoefu. Inakamata kila anayetaka kufanikiwa Upwork.
- Hii Kozi ipo tayari, sema inabidi iwe tailored. Bado nafikiria kuitafsiri kwa lugha pendwa ya hapa Bongo, Kiswahili. Ila, kutakuwa na option ya kiingereza na video zake kwa atakayehitaji. Ntaiweka kwenye platform ambayo itakuwa rahisi kulogin, kusoma na kuuliza maswali in drip content format (kwa mpangilio wa hatua kwa hatua).
- Napanga kuiundia video. Kwa sasa kozi ina text tupu. Nilifikiria kuweka vionjo, kulingana na uzoefu na interaction na freelancers wa hapa nyumbani, kwa lugha zote mbili kama nilivyotangulia kusema.
- Napanga kufanya personal analysis za account za Upwork. Jamaa humo ana service kabisa ya kukagua na kuboresha account. Nilipanga kukusaidia katika hilo.
- Mimi na hustler kama wewe. Nimetangulia kusema kwamba kozi hiyo aliiandika rafiki yangu. Na imeandikwa kwa lugha ya kiingereza. Mimi kazi yangu itakuwa kutafsiri, kuongezea vionjo na kukupa ili uelewe kirahisi.
Aidha, bado najitafuta. Nimepiga hatua kadhaa, lakini bado nairudia hiyo kozi na zingine ili kufanikiwa. Sijidai kuwa mbobezi kihivyo, bali kama aongozaye. Kozi imenisaidia, na nilitaka kukusaidia na wewe pia. Kumbuka, sio kila dereva barabarani anamiliki gari. (na kutomiliki kwake hakumfanyi kutostahili leseni).
- Kutengeneza content sio rahisi. Translation na localization inachukua muda na fedha. Itabidi muda wa kurekodi video, na kutafsiri, platform ya kupandisha kozi, na kuwasiaidia wadau waliokwama. (bila kusahau expenses za video na content hosting, ntakayolipia kwa mwezi/mwaka).
- Upwork hubadilika kila siku. Kozi hiyo ina zaidi ya miaka mitano (ila thamani bado ipo), na upwork huleta vionjo kila kuchao. Nilitamani kuhakikisha kuwa kozi inakuwa current, na vionjo vipya vinashughulikiwa na kuongezwa kama modules.
- Nilitamani tutengeneze community: Zaidi ya hapa JF, tuwe na kachama ketu kadogo ka watu wanaoupiga kule Upwork. Itakuwa private community. Kutakuwa na wabobezi na wageni humo. Wazoefu watatupa shuhuda za mafanikio.
Shuhuda zina nguvu ya kuhamasisha anayekata tamaa. Na pia, inaweza kutupa fursa ya kukutana na wabongo wenzetu wanaofanya kile ambacho tuna ndoto ya kukifanya.
- Maisha nje ya Upwork. baadaye, kwa wale ambao watakuwa wanataka maisha mengine, tutaongelea hili pia. Ila baadaye sana. (How to make direct clients, ambao nafanya nao kazi sasa).