Nafikiria Kuwashitaki PPF

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2009
Posts
5,101
Reaction score
1,952
Wana JF

Mimi ni mwananchama wa PPF, ninafikiria (na naamini nitaungwa mkono na wanachama wenzangu kwa hili) kuwapeleka mahakamani ili nihamishe michango yangu mahali pengine. Ni wanyonyaji wakubwa, wakati wanalipana mafao ya mamilioni kwa kufanyakazi miaka mitatu, bosi wangu alieanza kuchangia miaka ya 70 (alipata Masters na ACCA 1972 na akastaafu 2008) amelipwa chini ya Milioni 20 na pension yake ya mwezi ni 80,000).

Naomba msaada tafadhali wandugu tuondoe uonevu huu.
 
Malipo ya mafao yanategemea na mshahara wa mwanachama anayestaafu, hivyo ukienda PPF watakuonesha wanavyokokotoa mafao hadi kupata salio lako, baada ya kukata kodi of course.

Hata hivyo, labda kupitia SSRA (Social Security Regulatory Authority) watasaidia ku-harmonise pension benefits nk; kama utakumbuka SSRA imeanza kazi na juzi juzi tu Mkuu wa Kaya amezindua Bodi ya SSRA na sasa wameanza regulatory role yao, pengine itasaidia kutoa comfort kwa wanachama kwani Pension Entities wako na pesa nyingi sana. Moja ya promise ya SSRS ni kuwa wananchi/wanachama watakuw ahuru kujiunga na Mfuko wowote wa hifadhi ya jamii bila vikwazo wala mikwara yoyote.

Nakushauri nenda kawaone PPF (Members Srvices) utasaidiwa kabla kujaenda mahakamani, unaweza kukwama au kupoteza muda.
 
tatizo lipo kwetu wenyewe tena hasa watumishi wa umma na hasa serikali tunaoshangilia mishahara midogo na marupurupu mengi, hasara zake ni kukosa wekezo sahihi na kuishi maisha yasio sahihi

fikiria
 
Walioko kwenye hiyo authority wengi ndio hao hao walikuwa PPF sidhani kama kuna jipya ni mvinyo uleule kwenye chupa mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…