Nafikiria usaliti waliofanyiwa 'Hawa Ghasia na Kessy', hawa watu wawekwe chini ya uangalizi maalum wasije kujidhuru

Hakuna kitu kinauma duniani kama kujeuzwa mbuzi wa kafara.

Walichofanyiwa Kessy na Ghasia huenda kikawa kichomi kimoja kibaya sana kwenye maisha yao yaliobaki hapa duniani.

"Kwanini mimi? Kwanini mimi? Yaani ina maana sina thamani kiasi hicho mpaka wanitose mimi baharini? Yaani kati ya viti zaidi ya mia mbili, wameona mimi ndo sina maana?"

Amini nakuambieni, hakuna jambo linaloumiza mwanadamu hapa duaniani kama kuanza kujiuliza "Kwanini mimi, na sio wengine?"

Kutolewa kafara ni pigo kubwa sana la kuumiza nafsi.

Nashauri Hawa Ghasia na Kessy, wawekwe chini ya uangalizi maalum wasije kujidhuru.

Pamoja na kwamba watanzania wengi tumeumizwa na huu uchaguzi, ila navofikiri kuvaa viatu vya wabunge hawa wawili na wengine wachache wa CCM wataotolewa kafara, nabaki kujifariji kwamba 'matatizo ya binadamu ni mzunguko, yasipokutokea leo yatakutokea tu siki moja kwa namna tofauti'
Mlikuwa mnabwekabweka sana humu JF wakati wa kampeni na kejeli nyingi kwa CCM.Leo mambo ndiyo hayo tena CCM juu,mnaanza kuingilia mambo ya akina Hawa Ghasia ba Kessy. HAYAWAHUSU
 
Wala si hivyo...

Kwani Hakuna Lenye mwanzo likakosa MWISHO....

Wamekuwa wabunge wazuri kwa vipindi tofauti na mchango wao utakumbukwa Vyema...

Mama yetu Ghasia ameshika nafasi kubwa na nyeti....
Mzee wetu,sahibu yangu Ally Kessy ametuwakilishia vyema chama pale mjengoni na tutamkumbuka kwa kauli yake ya "tutamlazimisha ATAKE ASITAKE..."

Kudos Mama Hawa Ghasia
Kudos Comrade Ally Kessy.
 
Washakula sana bwashee,Hawa Ghasia keshakuwa mbunge na waziri keshakula sana acha na wengine wale.
Kesi nae piakeshakula sana kwenye ubunge na umri unamtupa mkono apishe na wengine pia wale.
 
HAWA AMEWATOA SADAKA ...BAADA YA AIBU YA WABUNGE 100% LAKINI HAISAIDII....TAARIFA ZA UHAKIKA NI KUWA KWENYE VITUO VINGI VILIVYOHESABU KURA KIHALALI KABLA YA AMRI YA KUJAZA KURA BANDIA HATA BILA KUHESABU ....jpm alikuwa ameachwa mbali sana ....sana , kuna baadhi ya sehemu chache walihesabu kura angalieni nao mtaona range ya matokeo ambayo ilikuwa ni predictive ya matokeo halisi baada ya huo muelekeo na kuonekana maeneo mengi kura bandia zilishindwa kuchomekwa kwakua zilikamatwa ., waliopewa kushindwa kazi na ikiwemo sehemu nyingine baadhi ya askari na wasimamizi wengine kuvujisha siri kwa wananchi IKATOKA amri kuwa hakuna tena kuhesabu bali ...maafisa walioandaliwa walipewa maelekezo ya kujaza matokeo ya kupika katika hali ya panic ...hii imesababisha maeneo mengi kura kuwa nyingi mara dufu ya watu waliojiandikisha kwenye eneo husika .......na asilimia kuzidi ..
HII IMEKUWA AIBU AMBAYO HATA WANA CCM ASILI INAWAUMA NA WANAONA AIBU KWA HAYA MATOKEO
Wasimamizi wa uchaguzi ni mabubu hawawezi kusema kitu, yaliyotokea hawawezi kuyasema, wameamua kunyamaza, hata nimgekuwa Mimi ningenyamaza
 
Washakula sana bwashee,Hawa Ghasia keshakuwa mbunge na waziri keshakula sana acha na wengine wale.
Kesi nae piakeshakula sana kwenye ubunge na umri unamtupa mkono apishe na wengine pia wale.
Mkuu inaonekana kuna ulaji huko.
 
Serikali ya ccm ina nafasi nyingi za kula bata na kufurahia maisha tutawapangia nafasi nyingine
Watapewa ukuu wa wilaya japo ubunge ni mtamu zaidi
Wakuu wa mikoa wenyewe wanataka ubunge
 
WATANZANIA TUJIANDAE KWA MAISHA MAGUMU KUPITA KIASI ...TUNAENDA KUONDOLEWA RASMI KWENYE DUNIA YA KISTAARABU AMBAYO TULIKUWA NA NDOTO YA KUIFIKIWA NA KUWEKWA KUNDI MOJA NA NCHI ZA HOVYO DUNIANI ...ZISIZOKUWA NA USTAARABU ...

MFANO HUWEZI KUSEMA KISIWA KAMA PEMBA UNASHINDA NA SIO STRONG HOLD ...DYNAMIC YA SIASA IKO HIVYO HAKUNA CHAMA DUNIANI KINAWEZA KUKUBALIKA SEHEMU ZOTE KWENYE NCHI ....BALI DEMOKRASIA HUWA INATAKA MAJORITY ...ALICHOKUWA ANALAZIMISHA JPM NI KUTAKA KUSHINDA KWA NGUVU HADI KWENYE MAENEO AMBAYO CCM HAINA USHAWISHI ..NA KUSAHAU UKWELI KUWA HIYO NDIO SIASA HUWEZI KUPENDWA KILA MAHALI HATA UWE MALAIKA
Hâta Uwe mungu huwezi pendwa
 
HAWA AMEWATOA SADAKA ...BAADA YA AIBU YA WABUNGE 100% LAKINI HAISAIDII....TAARIFA ZA UHAKIKA NI KUWA KWENYE VITUO VINGI VILIVYOHESABU KURA KIHALALI KABLA YA AMRI YA KUJAZA KURA BANDIA HATA BILA KUHESABU ....jpm alikuwa ameachwa mbali sana ....sana , kuna baadhi ya sehemu chache walihesabu kura angalieni nao mtaona range ya matokeo ambayo ilikuwa ni predictive ya matokeo halisi baada ya huo muelekeo na kuonekana maeneo mengi kura bandia zilishindwa kuchomekwa kwakua zilikamatwa ., waliopewa kushindwa kazi na ikiwemo sehemu nyingine baadhi ya askari na wasimamizi wengine kuvujisha siri kwa wananchi IKATOKA amri kuwa hakuna tena kuhesabu bali ...maafisa walioandaliwa walipewa maelekezo ya kujaza matokeo ya kupika katika hali ya panic ...hii imesababisha maeneo mengi kura kuwa nyingi mara dufu ya watu waliojiandikisha kwenye eneo husika .......na asilimia kuzidi ..
HII IMEKUWA AIBU AMBAYO HATA WANA CCM ASILI INAWAUMA NA WANAONA AIBU KWA HAYA MATOKEO
Hili ndio tatizo kuu la wanamageuzi humu jf na kwenye mitandao mingine.
1. Dharau. Acheni dharau na kufikiri ninyi ni bora kwenye kufikiri kuliko wengine na kudhani mawazo yenu ndo bora kuliko ya wengine hasa ya wana CCM.

2. Ujuaji. Hii kitu inawamaliza sana, acheni kujifanya mnajua sana wakati hamjui...

3. Jazba. Hili tatizo sijui linasababishwa na nini? We msikilize mwanaccm akiongea afu msikilize mwanamageuzi akiongea, utaona tofauti. Unamfokea nani? Hata kama unaeleza jambo la msingi, kama unafoka hakuna hatakae kuelewa.

4. Siasa na Harakati.....hapa wanamageuzi ndo mmefeli kabisa..huwezi kuleta uhanarakati kwenye siasa ukafanikiwa, kila siku utapigwa kwenye chaguzi.

5. Vitu na Watu.......hapa mlichemsha mapema sana, MTU hawezi kuendelea kama VITU havijaendelea...ili watu waendelee kwenye afya,ni lazima vitu kama hospitals na vifaa tiba ndo vianze kuendelea kabla ya mgonjwa. Ili mkulima aendelee ni lazima barabara iendelee kwanza.

5. Misingi.....tofauti kubwa kati ya CCM na vyama vingine ni misingi ya vyama vyao....CCM ina misingi imara kuanzia ngazi ya shina hadi taifa wakati huku kwingine ni shida....hata uongozi ngazi ya Mkoa hakuna.

6. Sera ya Majimbo....the biggest ever blunder once made by opposition side particularly Chadema, mindsets ya watanzania ipo wazi, Sera ya majimbo ni kujitenga na wao wamezoea umoja kupitia ujamaa...lazima uanguke.

7. Solidarity....hakuna umoja kati yao, wapo kimaslahi,kuing'oa CCM madarakani ni long term process, huwezi ukatoka zako huko Ubelgiji afu uing'oe CCM over a night...impossible.

8.Ukawa....we jiulize,kwanini ukawa ulikufa? Kwanini usiendelee na mwaka huu..wagombea 14 Wa upinzani against CCM wote hao Wa nini? Mnamchanganya mpiga kura, at the end anaamua kubaki na zimwi lake.

9. ACT Conflict.....unajiuliza why ACT waligombana,tena hadharani..Zitto na Maalim Seif against Member wakati wiki Mbili nyuma walimpamba maua? Wapinzani hawaaminiki.

10. Legends Wa Vyama......kwenye kampeni ni muhimu sana kuwashirikisha legends Wa vyama...Lissu kaenda moshi lakini Mzee mtei hakwenda...even Mbowe himself, chairman he didn't show up......nyie mnadhani ni issue ndogo lakini ina impact kubwa sana.

11. CCM ilijipanga......hapa ndipo upinzani ulimozikwa,this time CCM ilijipanga mno kupita Maelezo....chukua mfano Wa jimbo la Iringa mjini...watia nia wote akiwemo Steve Nyerere walishiriki kikamilifu kumpigia kampeni Jesca. Siku zote Msigwa alikuwa anashinda kwa msaada Wa wanaccm mwenyewe, CCM waliitilafiana wenyewe kwa wenyewe na Msigwa anafaidika,this time CCM walishikamana kupita maelezo.

Upinzani umeanguka lakini mnaweza mkasimama upya,though will take time probably 20yrs from now.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
 
Hakuna kitu kinauma duniani kama kugeuzwa mbuzi wa kafara.

Walichofanyiwa Kessy na Ghasia huenda kikawa kichomi kimoja kibaya sana kwenye maisha yao yaliobaki hapa duniani.

"Kwanini mimi? Kwanini mimi? Yaani ina maana sina thamani kiasi hicho mpaka wanitose mimi baharini? Yaani kati ya viti zaidi ya mia mbili, wameona mimi ndo sina maana?"

Amini nakuambieni, hakuna jambo linaloumiza mwanadamu hapa duaniani kama kuanza kujiuliza "Kwanini mimi, na sio wengine?"

Kutolewa kafara ni pigo kubwa sana la kuumiza nafsi.

Nashauri Hawa Ghasia na Kessy, wawekwe chini ya uangalizi maalum wasije kujidhuru.

Pamoja na kwamba watanzania wengi tumeumizwa na huu uchaguzi, ila navofikiri kuvaa viatu vya wabunge hawa wawili na wengine wachache wa CCM wataotolewa kafara, nabaki kujifariji kwamba 'matatizo ya binadamu ni mzunguko, yasipokutokea leo yatakutokea tu siki moja kwa namna tofauti'
Spin doctor wanacheza na akili zenu tu, na nyinyi mlivyo wepesi mmeshaingia king.

Kweli kumtawala mtanzania ni kazi nyepesi sana ndio maana magufuli amawapelekesha kama gari bovu.
 
Kwani umesahau kwamba kuna Wakuu Wa Mikoa, Wakurugenzi na Ma DC ambao walivyotia nia tu walitumbuliwa na wapo waliolindwa wakala mshahara na Magufuli aliwapigia kampeni!??

Hakuna kitu kinauma duniani kama kugeuzwa mbuzi wa kafara.

Walichofanyiwa Kessy na Ghasia huenda kikawa kichomi kimoja kibaya sana kwenye maisha yao yaliobaki hapa duniani.

"Kwanini mimi? Kwanini mimi? Yaani ina maana sina thamani kiasi hicho mpaka wanitose mimi baharini? Yaani kati ya viti zaidi ya mia mbili, wameona mimi ndo sina maana?"

Amini nakuambieni, hakuna jambo linaloumiza mwanadamu hapa duaniani kama kuanza kujiuliza "Kwanini mimi, na sio wengine?"

Kutolewa kafara ni pigo kubwa sana la kuumiza nafsi.

Nashauri Hawa Ghasia na Kessy, wawekwe chini ya uangalizi maalum wasije kujidhuru.

Pamoja na kwamba watanzania wengi tumeumizwa na huu uchaguzi, ila navofikiri kuvaa viatu vya wabunge hawa wawili na wengine wachache wa CCM wataotolewa kafara, nabaki kujifariji kwamba 'matatizo ya binadamu ni mzunguko, yasipokutokea leo yatakutokea tu siki moja kwa namna tofauti'
 
Ghasia Ndiyo Aliambiwa Korosho Zitakuponza
Kessy Alikuwa Garasa Chamani Muda Mrefu
 
Watanzania wengi wamefurahishwa na uchaguzi huu uliopita....hao uliowataja wameachwa kwa sababu hawakuwa na msaada na chama chao.
 
Back
Top Bottom