Nafikiria usaliti waliofanyiwa 'Hawa Ghasia na Kessy', hawa watu wawekwe chini ya uangalizi maalum wasije kujidhuru

Nafikiria usaliti waliofanyiwa 'Hawa Ghasia na Kessy', hawa watu wawekwe chini ya uangalizi maalum wasije kujidhuru

Serikali ya ccm ina nafasi nyingi za kula bata na kufurahia maisha tutawapangia nafasi nyingine
Hilo ni la kweli, kwa wateule wachache ambao ni 0.00001% wanashangilia ushindi wa kijambazi kwakuwa wana jua wana nemeka na mfumo!! Lakini kuna wale ambao, wanatumika tu kwa hao wachache, kuiba kura, kudhuru wengine eti ccm kindakindaki, hata kula yao kwa siku ni mtihani, ndio wakuonea huruma!! Leo bila kujua anashabikia bunge kuwa la chama kimoja!!!
 
Wata move on tuu... Ni kawaida sana...

Kama ni hivyo basi angepagawa Wasira...



Cc: mahondaw
 
Hili ndio tatizo kuu la wanamageuzi humu jf na kwenye mitandao mingine.
1. Dharau. Acheni dharau na kufikiri ninyi ni bora kwenye kufikiri kuliko wengine na kudhani mawazo yenu ndo bora kuliko ya wengine hasa ya wana CCM.

2. Ujuaji. Hii kitu inawamaliza sana, acheni kujifanya mnajua sana wakati hamjui...

3. Jazba. Hili tatizo sijui linasababishwa na nini? We msikilize mwanaccm akiongea afu msikilize mwanamageuzi akiongea, utaona tofauti. Unamfokea nani? Hata kama unaeleza jambo la msingi, kama unafoka hakuna hatakae kuelewa.

4. Siasa na Harakati.....hapa wanamageuzi ndo mmefeli kabisa..huwezi kuleta uhanarakati kwenye siasa ukafanikiwa, kila siku utapigwa kwenye chaguzi.

5. Vitu na Watu.......hapa mlichemsha mapema sana, MTU hawezi kuendelea kama VITU havijaendelea...ili watu waendelee kwenye afya,ni lazima vitu kama hospitals na vifaa tiba ndo vianze kuendelea kabla ya mgonjwa. Ili mkulima aendelee ni lazima barabara iendelee kwanza.

5. Misingi.....tofauti kubwa kati ya CCM na vyama vingine ni misingi ya vyama vyao....CCM ina misingi imara kuanzia ngazi ya shina hadi taifa wakati huku kwingine ni shida....hata uongozi ngazi ya Mkoa hakuna.

6. Sera ya Majimbo....the biggest ever blunder once made by opposition side particularly Chadema, mindsets ya watanzania ipo wazi, Sera ya majimbo ni kujitenga na wao wamezoea umoja kupitia ujamaa...lazima uanguke.

7. Solidarity....hakuna umoja kati yao, wapo kimaslahi,kuing'oa CCM madarakani ni long term process, huwezi ukatoka zako huko Ubelgiji afu uing'oe CCM over a night...impossible.

8.Ukawa....we jiulize,kwanini ukawa ulikufa? Kwanini usiendelee na mwaka huu..wagombea 14 Wa upinzani against CCM wote hao Wa nini? Mnamchanganya mpiga kura, at the end anaamua kubaki na zimwi lake.

9. ACT Conflict.....unajiuliza why ACT waligombana,tena hadharani..Zitto na Maalim Seif against Member wakati wiki Mbili nyuma walimpamba maua? Wapinzani hawaaminiki.

10. Legends Wa Vyama......kwenye kampeni ni muhimu sana kuwashirikisha legends Wa vyama...Lissu kaenda moshi lakini Mzee mtei hakwenda...even Mbowe himself, chairman he didn't show up......nyie mnadhani ni issue ndogo lakini ina impact kubwa sana.

11. CCM ilijipanga......hapa ndipo upinzani ulimozikwa,this time CCM ilijipanga mno kupita Maelezo....chukua mfano Wa jimbo la Iringa mjini...watia nia wote akiwemo Steve Nyerere walishiriki kikamilifu kumpigia kampeni Jesca. Siku zote Msigwa alikuwa anashinda kwa msaada Wa wanaccm mwenyewe, CCM waliitilafiana wenyewe kwa wenyewe na Msigwa anafaidika,this time CCM walishikamana kupita maelezo.

Upinzani umeanguka lakini mnaweza mkasimama upya,though will take time probably 20yrs from now.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
ongeza 12. KUTOJIFUNZA NAMNA YA KUIBA KURA ....KWANI HUWEZI KUSHINDA BILA UJANJA UJANJA NA WIZI
 
Walijua before wewe!

Huoni mada zimehamishiwa kwao wewe? Hakuna anayejadili juu ya akina Zitto, Mbowe n.k kuangushwa kwa magumashi bali mjadala umekuwa ni juu ya Kessy!

Subiri uone Kessy atapewa kitengo gani na huyo Hawa Ghasia!
Mfano huyo Mama watu hawamjui vizuri, ni threat moja kali sana kwenye kitengo!!
Mshaanza sana watoto wa mjini na kasumba za hooo huyu kitengo. Kila mtu mjanja au aliyezurumiwa ni kitengo ausio, Watoto wa mjini mnachosha
 
Back
Top Bottom