Nafsi inanituma nikafanye shughuli zangu geita na nitafanikiwa kimaisha

Nafsi inanituma nikafanye shughuli zangu geita na nitafanikiwa kimaisha

Kategele

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Posts
1,055
Reaction score
2,466
Habarini wana JF wezangu,
Poleni na hongereni kwa majukumu yenu ya kila siku kupambania kujinasua kimaisha, pia kukuza uchumi wa Nchi yetu.



Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 na kiwango cha elimu yangu ni Shahada, katika maisha yangu nilipanga kusoma mwisho level ya shahada tu (Uhandisi ujenzi) ambayo itanitosha kupambana na maisha yangu.


Nimeshaanza kupambana kimaisha si haba nilipofikia hapa ni jambo la kumshukuru Mungu ingawa ndoto zangu bado hazijatimia.


Nirudi kwenye mada,nafsi yangu inanituma niende Geita nikapambane nitafanikiwa kimaisha kwani nikiangalia umri wangu bado kama miaka 10 tu ya kupambana nikiwa na nguvu kutimiza ndoto zangu (Life begins at 40)

Naomba wenyeji wa geita mnijuze fursa zinazopatikana hapo mjini, hali ya maisha, pia fursa za kazi kwenye mgodi wa GGM na kampuni mbalimbali zinazofanya kazi mgodini.


Karibuni kwa ushauri wenu.
 
Back
Top Bottom