UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,753
- 12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!
Nawalaumu sana wazazi wangu na Mimi mwenyewe kutozaliwa/kuzaa nje ya Tanzania!
Sababu ya kwanza ni kwamba,hivi mzee wangu kweli alishindwa kupiga Swaga mwanamke yeyote wa Kikenya hadi azae Tanzania?,Ukizingatia kwetu hapo Tarime mjini hadi Sirari ulipo mpaka wa Kenya ni pua na Mdomo, napataga tu stori kwamba mzee wangu alikuwa na mademu lukuki wa Kikenya lakini ajabu hakuwahi hata kuzaa nao, huenda angezaa na hao mademu wa enzi zake Sasa hivi ningekuwa Mkenya nabonga zangu Ung'eng'e ulionyooka siyo kama huu wa kuunga unga ambao hata kuuongea hadi nikaze misuli ya makalio!
Pili, Upuuzi/Ujinga ambao na Mimi nimeufanya na nimekuja kushtuka miaka ya hivi karibuni, ni kuzaa na mwanamke wa Kitanzania, Aisee hii kitu inaniumiza sana na najua wanangu pia watakuja kunilaumu sana kama ambavyo Mimi namlaumu Dingi!
Kiukweli Hawa watoto wangu wawili wananitosha kabisa na siku Nilitaka watoto wengine nitajitahidi nisizae na mwanamke wa Kitanzania, Lengo langu ni hadi kufikia Mwaka 2030 nisiwe hapa nchini, napambana kutafuta pesa nisepe maana nikiendelea kukaa hapa nitashawishika na wanawake wenye Vyungu vikubwa hatimaye utashangaa nazama kuchota maji matokeo yake ni "Mbembeleze huyo mtoto"
Sababu ya Mimi kufanya hivyo ni kutotaka kuwarithisha wanangu huu ujinga/uzumbukuku wa wananchi wa hii nchi! Unaweza kuzaa mtoto mwenye akili lakini kama atasoma na kuzungukwa na mazumbukuku ni lazima na yeye atakuwa Zumbukuku tu!
Kilichofanya ndugu zangu kuandika huu Uzi Kwa Uchungu ni namna ambavyo nafuatilia wananchi ambavyo wanaendelea kutoa maoni kwenye huo mpango wa Serikali uitwao "DIRA YA MAENDELEO" . Yaani kiukweli unawasikiliza Watanzania namna wanavyotoa maoni hadi najiuliza ni nani aliyeturoga Watanzania? Hivi kweli suala la Watoto kuimba nyimbo za Zuchu ni la kwenda kusimama mbele ya hiyo kamati na kuliwasilisha kama hoja ya dira ya Maendeleo? Kweli? Hivi ni wapi tulikosea kama Taifa?
Yaani badala wananchi watoe mapendekezo konki ambayo yatalisaidia Taifa kupiga hatua za Kimaendeleo wao wanaleta hoja za Kijuha! Aisee nimesikitika sana dadeeeeki!
Kuna mwengine nadhani ni kiongozi wa dini, yeye kapendekeza kabisa ya kwamba Viongozi wa dini walipwe mshahara kila mwezi Tsh 900,000/=, Nilitegemea huyo kiongozi wa dini angekuja na hoja ya kwamba, maslahi yaboreshwe Kwa Madaktari, walimu na watumishi wengine Ili kuleta uwiano uliobora katika kada za watumishi lakini yeye anakuja na hoja kijinga,Viongozi wa dini pamoja na kiwalaghai Watanzania Hawa mazumbukuku Kwa kujipatia fedha nyingi lakini bado hawatosheki!,Nilitegemea angejenga hoja ya kwamba,watumishi wote wa kidini walipe Kodi na ushuru mkubwa badala yake anakuja na hoja za kizumbukuku!
Aisee Kuna namna yawezekana hili Taifa tulimkosea chief Bulito na huenda hata Nyerere kabla ya kufa aliacha laana kwenye hili Taifa, Benjamin Mkapa alipaswa atueleze ukweli huenda alikuwa anajua ila akakausha kila mtu afe kivyake!
Kinachonitesa ndugu zangu Mimi Nina akili nyingi mno nadhani hadi zinakaribia kumwagika, Sasa kukaa katikati ya mazumbukuku na akili zangu nyingi napata taabu sana! Kungekuwa na uwezekano wa kuwagawia akili baadhi ya watanzania ningefanya hivyo lakini haiwezekani!