Nagombea Remote na Watoto!

Nagombea Remote na Watoto!

mikela, kununua tv nyingine na kuhamia chumbani haina tofauti na kuhama nyumba kwa sababu tu ya kutofautiana kitu na mwenzio/wanao. kama baba kuna umuhimu wa kujua wanao wanaangalia nini, na wanafanya nini wawapo nyumbani. hii ina maana na baba pia ata-sacrifice kutoangalia mpira na boxing, na mama nae na movies zake pia ziwe rehani. pia ni muhimu kufundisha watoto kushare resources na watu waliopo nyumbani kwao. kuna watu ofisini ukisafiri nao humo garini atataka msikilize kwaya yake tu (anakuja na cd kabisaa), mle hoteli aliyoizoea na kulala anapotaka yeye! nadhani kunaanzia huku. wafundishe wanao kuwa tunaweza kuangalia cartoon, na national geographic wajifunze kitu pia. na ccn ili wajue world news. humo kwenye movie za kiswahili na ki-nijeria nisitie neno manake sioni watakachojifunza zaidi ya miondoko feki na english mbobu, ila inahitaji kuwashawishi pia!
hata kama unanunua tv ya chumbani ni kwa ajili ya kuangalia news za alfajiri wakati unamuwinda mama nanilii kwa morning glory. sio kwa ajili ya kukimbia wanao na cartoon. ni mtizamo tu lakini...

Marvelous point!!
 
Pole kaka...wape watoto nafasi ya kuangalia kile wanachoona kinawafaa...sidhan kama muda wote watoto wanakuwa wamekodolea macho kwenye TV. kuna muda kuangalia news..hapo wote lazima muwe tayari...kuna muda watoto wanafanya Homework au tayari wamelala...hapo unaweza kujinafasi...kununua TV ingine sio solution...solution ni kutokuweka ubinafsi kwenye TV..chaneli iliyopo wote angalien..kuna pia uwezekano wakuwashawishi watoto taratibu kuwa na mazoea ya kuangalia chaneli zote na taratibu watakuunga mkono...kwa mtazamo wangu TV nyumbani kuwepo mara nyingi ni kwa watoto na wanashinda nyumbani. kwa sisi akina baba mara chache...basi kwa kumaliza kusema hayo...kama unaona huwezi kabisa kabisa kuwashawishi watoto basi fanya mpano weka TV ingine chumbani ili uipe roho yake ile kitu inapenda..kama ni mpira utaweza kuangalia.....mama watoto nae akijisikia kuangalia anaweza kufanya hivyo pia...ili hali watoto wanajinafasi na yao sebuleni.
 
NN, watoto ni muhimu kujifunza discipline. wangu hawatapata taabu coz i lov popeye, the penguins of madagascar na tom & Jerry,lol. Ila uzuri cartoons like all dstv programs, kwa siku zinarudiwa several time bt kuna series or mpira havina utamu kuangalia marudio. u shld be able to negotiate nao,we watch cartoon up until this time, then ball, then movie.. wakileta mchezo saa ya mpira wasiposaidia jikoni basi itakua homework if nt cleaning their room,lol! I miss me mom kwa kweli,hahahah!
Ni kweli King'asti. Ila sasa bora lipi? Uwanyime kabisa uhondo watoto au uwape uhondo robo tabu? Mimi nadhani kama watoto wanaangalia vikaragosi wanakuwa hawako interested sana maneno. Kwanza vikaragosi vingi haviongeagi. Angalia Tom and Jerry kwa mfano. Wao ni kufanyiana. Longo longo hakuna. Sasa hapo baba unaweza ukawa unaangalia Nightline ABC huku wao wakimwangalia Spongebob Square Pants kwenye Cartoon network na wote mkafaidi na kuridhika.
 
yaani hii mada ilikuwa nzuri mno....

kuna suala la mtoto mmoja nae kushika remote control.....wenzie hawana sauti.....hilo nalo pia..
 
kakaaa we ni rais wa nyumba yako,watoto watakuwa vichwa maji kuangalia tv
mda mwingi,wape mda mfupi wakitoka shule wapunzike kidogo then homework
cartoon wasiangalie zaidi ya saa moja,wakisha kula wakajisomee study room kama ipo
afu walale walau saa 4.tv inaharibu sana watakuwa wajinga hasa hizi tamthilia,filamu hizi
na pia kama ni DSTV kuna program lock unaweka password hawawezi kuona baadhi ya channels
wadekeze afu uvune mabua.
 
Hapo kwenye red n bolded: kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Huko juu umetoa ushauri mzuri ila ndo umemalizia kwa mcharuko haswaaaaaa!
unajua mkuu nakushangaa kwa kuwa unaomba ushayri kwa simple and obvious. some things just need common sense. sasa kweli kama jambo ndogo kama hili linakuktatiza na mengine je yakitokea si utahama boma mkuu wangu.
 
Mm nnaishi na wadogo zangu<sio watoto> nlikuwa nakereka sana pale napotaka kuangalia labda This week in perspective ya tbc na wao wanataka kuangalia music eatv na dtv! Nilipojaribu kuwaelimisha walijifanya wamenielewa lakin nikagundua hawajaridhia kwan hata nikiwaachia waangalie vipind vyao inapofika muda wa kutizama program zangu wanaondoka wote na kubakia peke yangu(kususa) nikanunua tv ya chumban sasa hakun tatizo!
 
Hili wala siyo tatizo mbona...

Wewe nunua tivii yenye feature ya Picture in picture. Ukiwa nayo ya hivyo wewe unaweza ukaangalia vipindi vyako huku na wao wakijinafasi na akina Pink Panther au Popeye the sailor man na wote mkawa mko kwenye sofa mkiangalia.

Ahha hhaa, umenigusa mwenzangu, mtoto akainza kukodolea hizo hata umweteje hageuki ni hatari kweli...
 
Back
Top Bottom