Nahamia Burkina Faso

Nahamia Burkina Faso

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814

View: https://youtu.be/hHvbungjv-I?si=WvGqWz5ugZWo4yrY

Kuna wakati Mtanzania hakuwa anashughulishwa na tumbo lake tu: kufikiria atalipiaje kilo ya sukari, atalipiaje maji, umeme, gesi.... zote bidhaa muhimu kwa maisha lakini zimewekewa VAT ya kiwango cha juu (Value Added Tax. Hata hawajui maana yake!).

Wakati huo Watanzania walikuwa wanaishi 'maadili makuu': ukombozi wa Afrika, Umoja wa Afrika, Udugu wa Mwafrika, heshima ya Mwafrika, Mitindo ya Mwafrika, Utamaduni wa Mwafrika, nk. Wakati huo kwa kweli tulikuwa na uongozi uliopata mwanga wa elimu ya kweli (siyo utitiri wa madokta na waheshimiwa wasio na heshima hivi leo), kiasi kwamba Mtanzania wa kawaida kabisa barabarani anaweza kukukalisha chini kitako akakuelezea yanayoendelea Zambia, Senegal, Egypt, Congo-Brazzaville..... kwa sababu watu walikuwa na mwamko wa ufahamu, elimu, kutaka kujua.... na si tumbo tu. Leo kati ya Watanzania kumi waliohitimu Chuo Kikuu utakaowauliza jina la mji mkuu wa Madagascar, utakuwa umebahatika wawili wakikujibu sahihi!

Zama hizo, akili za Watanzania zilikuwa na uhai, na waliishi 'full life', maisha ya akili na pia ya mwili.

Tafadhali usinifahamu vibaya kwamba hatukuwa na shida zetu, no, zilikuwepo. Hazikuwa kubwa kama sasa, kwa vile hata hao viongozi walikuwa wanaishi maisha ya kawaida- hilo kwa ajabu kubwa, lilipunguza makali.

Ila Tanzania imeyatupa yote haya kwa sababu ya ukuwadi wa soko huria na kuchumia tumbo na.... Tanzania si kinara tena wa udugu wa Afrika. La, mwenge huo sasa unachukuliwa na kapteni mdogo IBRAHIM TRAORE. Katika kikao chake na ujumbe wa Diaspora kutoka Marekani na Caribbean, Traore (tazama video) aliwaambia 'mtu yeyote mweusi Burkina Faso ni kwao' na kwamba ingawaje ujumbe huo ulipewa vitisho na Marekani kwamba wasikanyage Burkina, ila umeamua kupuuza vitisho hivyo, na kwa kufanya hivyo ujumbe umetoa ilani kwa diaspora wote wasisikize maneno ya kukatisha tamaa na wasonge mbele katika kuwaunganisha Waafrika. Tazama washiriki wanavyozungumza kwa jazba na jaha, na upendo mkuu wa ujumbe wa Le capitaine!

Sisi tusioishi kwa ajili ya matumbo tu, magari ya V9, apartment Dubai na akaunti Marekani..... tunaona Burkina Faso kuna maisha ya 'mwanga wa akili' tofauti na 'giza la tumbo' tunaloliishi huku. Kwa kwenda Burkina Faso, kabla hawajamwua le capitaine Ibrahim Traore naona nitarudisha 'full' uhai wangu. Nimeamua hata kutongojea kikokotoo chao kipya!
 
UMESEMA KWELI TUNA SEC ZA KATA NA VYUO VIKUU VYA KATA
 
Back
Top Bottom